MAWAZIRI 30 WA AFRIKA WAIPITISHA TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA KIMATAIFA WA 65 WA UTALII 2022
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania Paris, Mhe. Samweli Shelukindo (kushoto) pamoja na Waziri wa Utalii wa Sao Tome, Carlos Gomes wakifuatilia wakati Rais wa Cape Verde, Dkt. Jorge Carlos Fonseca,akifungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Waziri wa Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe.Lela Mohamed Mussa ( wa kwanza kulia) akiwa pamoja na baadhi ya maofisa alioambatana nao wakimfuatilia Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) Bw. Zurab Pololikashvil wakati alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na shirika hilo UNWTO katika mkutano unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, ambapo amezitaka nchi za Afrika kufanya utalii kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa nchi zake kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt ,Damas ndumbaro akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) huku akiwa amembatana na wajumbe wengine ambao ni Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, Kamishna Uhifadhi kutoka TAWA, Mabula Misungwi, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga , Balozi wa Tanzania Paris, Mhe. Samweli Shelukindo pamoja na maofisa kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) , TTB pamoja na TANAPA
Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo akiwa apmoja na Kamishna Uhifadhi kutoka TAWA, Mabula Misungwi, wakiwasikiliza Wadau wa makampuni ya kutangaza utalii wakati walipokuwa wakiwasilisha mada zao katika Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na shirika hilo UNWTO katika mkutano unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Waziri wa Utalii wa Gambia, Hamat Bah mara bada ya kufunguliwa rasmi kwa Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendela kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo mwakani.
Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UNWTO), Zurab Pololikashvili amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kuhakikisha Afrika inafanya vizuri katika masuala ya utalii ili kuongeza ajira kwa wananachi wenye nia ya kutaka kujihusisha na shughuli ho ya Utalii
Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UNWTO), Zurab Pololikashvili amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa ni kuhakikisha Afrika inafanya vizuri katika masuala ya utalii ili kuongeza ajira kwa wananachi wenye nia ya kutaka kujihusisha na shughuli ho ya Utalii
Baadhi ya Mawaziri wa Utalii Barani Afrika wakiwa pamoja na Watalaamu ktutoka Shirika la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani(UNWTO) wakifuatilia mada mbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa masuala ya utali na mbinu ambazo nchi za kiafrika zinatakiwa kufanya ili kwenda sambamba na soko la utalii hasa katika kipindi hiki ambacho sekta ya utalii imeedhoofu kutokana na uwepo wa ugnjwa wa corona
Rais wa Cape Verde, Dkt. Jorge Carlos Fonseca akiwa kenye picha ya pamoja na Mawaziri wa Utalii Barani Afrika mara baada ya kufungua mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, wa tatu kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Cape Verde.
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) limeichagua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa 65 wa Kanda ya Afrika utakaofanyika Jiji la Arusha Oktoba,2022.
Mkutano huo, utajumuisha Mawaziri wote wa Utalii wa Bara la Afrika huku ukitarajia kuongeza tija kwa Tanzania kwenye fursa za kukuza Utalii Kimataifa.
Akizungumza jana nchini hapa katika kisiwa cha SAL, Cape Verde, katika mkutano huo wa siku Nne mbele ya zaidi ya Mawaziri 30 wa utalii, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewashukuru Mawaziri hao kwa kuipa heshima nchi ya Tanzania huku akiowaomba mawaziri wote wa utalii kuja kushiriki katika mkutano huo mwakani.
Katika uchaguzi huo uliowakutanisha mawaziri 30 wa utalii wa Bara la Afrika, Mawaziri hao waliridhia kwa kauli moja kuwa Tanzania ina sifa zote za kuwa mwenyeji wa mkutano huo mara baada ya Tanzania kuwa nchi pekee iliyokuwa imeonesha nia ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Kufuatia hali hiyo Tanzania inakuwa ni nchi ya kwanza kupita bila kupingwa na katika mkutano wa Kimataifa wa utalii wa 64.
Akizungumzia manufaa ya mkutano huo, Dkt. Ndumbaro amesema kufanyika mkutano huo nchini utaiweka Tanzania katika ramani ya dunia kwa kutangaza fursa uwekezaji katika sekta ya utalii pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema kitendo cha Mawaziri wote kuridhia kwa kauli moja kuwa Tanzania iwe mwenyeji wa mkutano huo ni imani kubwa ya waliyonayo kwa nchi ya Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla
Dkt. Ndumbaro amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ni hatua mahsusi kwa nchi kujitangaza kimataifa kwa vile washiriki mbalimbali duniani watahudhuria mkutano huo wakiwemo wabobezi wa utalii pamoja na makampuni makubwa ya kutangaza vivutio vya utalii kutoka nje yatatangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na Afrika kwa ujumla
Kwa upande wake Waziri wa Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema utachagiza idadi ya watalii watakaoitembelea Tanzania kupitia mkutano huo.
” Tunajisikia fahari kuona ajenda yetu kama nchi ya kuja kushiriki katika mkutano huu umefanikiwa na tuna matumaini makubwa kuwa mkutano huo utatangaza vivutio vya utalii vilivyoko Zanzibar na Tanzania bara”. alisisitiza Mhe. Lela Mussa.
Aidha, Katika mkutano huo Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Bajeti na Mipango ya UNWTO kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu kuanzia sasa.
Naye Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvili amesema katika kipindi chake cha uongozi moja ya kipaumbele chake kikubwa ni kufanya uwekezaji katika bara la Afrika ili kuongeza ajira kupitia sekta ya utalii.
Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano huo unaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ambaye ameambatana na Waziri wa Utalii na Mambokale wa Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa
Pia Wajumbe wengine walioambatana na Mhe. Waziri ni pamoja Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, Kamishna Uhifadhi kutoka TAWA, Mabula Misungwi, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga , Balozi wa Tanzania Paris, Mhe. Samweli Shelukindo pamoja na maofisa kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) , TTB pamoja na TANAPA
No comments: