Chuo cha NIT chapongezwa kwa mipango yake ya kimkakati
Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) (kushoto) akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara kuhusu moja ya mfano wa ndege ambayo hutumika kufundishia wanafunzi kwa vitendo katika Chuo hicho mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara akizungumza na watumishi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam kuona ni namna gani wanatoa mafunzo.
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Prof. Zacharia Mganilwa akizungumza mara baada Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam na kuona ni namna gani chuo hicho kinatoa mafunzo.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara amekipongeza Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kutoa wataalamu bora katika sekta ya usafirishaji na kusema kuwa kinapaswa kuwa chuo cha serikali kwa kuzingatia elimu wanayoitoa.
Amesema, elimu inayotolewa chuoni hapo imekuwa chachu katika nchi yetu kwani wataalamu wanaozalishwa wamekuwa wakisimamia miradi mikubwa ya kisasa ya usafirishaji inayoendelea kujengwa hapa nchini na kukuza uchumi wetu.
Waitara ameyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es wakati wa ziara yake chuoni hapo ili kuangalia na kujadili maendeleo ya NIT na namna kinavyotoa Mafunzo yake.
Amesema, tangu alipoteuliwa kushika nyadhifa yake ya naibu waziri wa uchukuzi, ametembelea Taasisi zaidi ya 20 za Ujenzi na Uchukuzi ikiwemo kituo cha Hali ya Hewa Kigoma, lakini NIT kinafanya kazi kubwa na kimejipanga kwa kila kitu.
Amesema, alienda Kigoma Chuo cha Hali ya Hewa ila taarifa aliyopewa hakiuelewa kwani alitarajia kukuta vitu vikubwa na vya kisasa na watu wakiwa wamejipanga lakini haikuwa hivyo hivyo hali kadhalika na Chuo cha Bandari na kwenyewe hakulidhishwa na mambo yake, lakini amefika NIT ameona jinsi walivyojipanga.
Nimeona namna mlivyojipanga, profesa na timu nzima nawapongeza sana, sasa hiki ndicho chuo na kinapaswa kuwa cha serikali siyo vile vingine, nadhani sasa uvishauri vyuo vingine vya ufundi kuja kujifunza kutoka chuoni hapa" amesema Waitara.
Aidha amekipongeza huo hicho kwa kufanikisha ununuaji wa mitambo ya kisasa kwa juhudi zao binafsi na kuwataka kuendelea na hali hiyo siyo kama sehemu zingine unapewa maelezo ya vile vitu ambavyo serikali imepeleka.
“Chuo hiki hakijapata fedha kwa muda mrefu sana nadhani mwaka huu ndo kimepata milioni 500 lakini kupitia mapato yake ya ndani kimeweza kukusanya bilioni moja ni mara mbili ya fedha ambazo Serikali imetoa, na kiukweli tumetoa fedha baada ya kuona Mkuu wa Chuo na wenzake wanafanya kazi kubwa iliyotukuka,” amesema
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Prof. Zacharia Mganilwa amesema amesema uwekezaji mkubwa unaofanya na Serikali katika sekta ya usafirishaji umefanya chuo hicho kuendelea na mipango madhubuti ya kuzalisha wataalamu mahili watakaokuwa na elimu bora ya uweza
Amesema chuo kitahakikisha kinaendelea kutoa elimu bora ili kupatikane wataalamu katika sekta zite za usafirishaji yaani Anga, Barabara, Reli ya kisasa inayoendelea kujengwa na hata usafiri wa majini.
“Tunajua, Serikali inakarabati meli za kisasa na kununua zingine, tuna mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), inapanua bandari na kujenga barabara, tunaimani kupitia chuo chetu tutatoa wataalamu waliobobea na wenye uwezo wa kushindana katika masoko ya kimataifa,” amesema Profesa
Mganilwa.
Msimamizi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) Bw.Christian Nabora (wa kwanza kushoto)akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara namna ya kugundua gari lililokuwa na kasoro kupitia kompyuta maalumu baada ya kufanyiwa ukaguzi katika mashine maalumu mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) Bw.Christian Nabora (kulia)akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara namna wanavyopima magari kwa kutumia matambo maalumu na kuweza kugundua kasoro iliyopo kwenye gari lililokuwa na kasoro mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) (kushoto) akimuelezea Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara kuhusu namna engine ya ndege walionayo inavyosaidia kufundisha wanafunzi wa chuo hicho kwa vitendo mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
No comments: