MZIMU WA SIMBA WAZIDI KUITESA YANGA MICHEZO YA KIRAFIKI.
Na Abdullatif Yunus.
Wakati Timu mbalimbali za Soka zikiendelea na Usajili wa Wachezaji wapya katika Vikosi vyao hapa Nchini kabla ya Ligi kuu kuanza kutimua Vumbi kwa Msimu ujao wa 2021-2022, Simba imeonekana wameonekana kuendelea kuionea Timu ya Yanga kwa vichapo mbalimbali.
Mwishoni mwa Wiki Jana umechezwa mchezo wa Soka uliokutanisha Mashabiki wa Simba na Yanga wanaounda Timu ya Mpira ya Bukoba Veterans yente Makao Makuu yake Bukoba Manispaa, mchezo uliomalizika kwa Timu ya Simba kuibuka na Ushindi wa bao Mbili kwa nunge.
Mchezo uliochezwa katika kiwanja Cha Kaitaba Ulihudhuriwa na Mashabiki, wapenda soka pamoja na Viongozi mbalimbali huku Mgeni Rasmi katika mchezo huo akiwa Ni Mkuu wa Wilaya za Bukoba Mhe. Moses Machali.
Akitoa Salaam zake Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Mhe. Machali amepongeza mchezo huo na Waratibu wa Tukio Hilo,huku akisisitiza Michezo ni furaha, Michezo ni Upendo na Michezo ni Afya, hivyo wananchi hawana budi kuendelea kuipa kipaumbele Michezo ambayo pia ni sababu mojawapo ya kuimarisha miili ili kujikinga na magonjwa nyemelezi.
Itakumbukwa kuwa Mchezo wa Mwisho kuzikutanisha Timu za Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu, Simba wakiondoka na alama Tatu baada ya kuifunga Yanga Goli Moja. Mchezo wa Kaitaba wa mashabiki wa Simba na Yanga uliandaliwa na kuratibiwa na Ndg. Hussein mtumishi kutoka Taasisi inayojihusisha na kulea na kuendeleza vipaji shuleni ijulikanayo Kama Jambo Bukoba.
Sehemu ya Kikosi Cha Mashabiki wa Yanga kinachounda Timu ya Bukoba Veterans Kama kinavyoonekana katika picha ya Pamoja.
Mkuu wa Wilaya za Bukoba Mhe. Moses Machali akizungumza na Wachezaji Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki wa Mashabiki wa Simba na Yanga Uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Muonekano wa Zawadi ya Kikombe walichojinyakulia Timu ya Mashabiki wa Simba Mara baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Yanga.
Pichani Mkuu wa Wilaya za Bukoba Mhe. Machali akikabidhi Kombe Hilo kwa washindi.
Timu ya Mashabiki wa Simba wanaounda Kikosi Cha Bukoba Veterans wakisherehekea Ushindi wao Mara baada ya Kushinda mchezo wao.
No comments: