MBIO ZA MWENGE MAALUM ZACHANJA MBUGA KIBAHA UKITOKEA BAGAMOYO
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WILAYA ya Kibaha imemkabidhi ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,LT.Josephine Mwambashi ,madawati 50 kisha kuyakabidhi kwa halmashauri ya Mji wa Kibaha wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha.
Akikabidhiwa madawati hayo wakati wa uzinduzi wa madarasa matano katika shule ya msingi Mtongani ,wilayani Kibaha ,alisema ni muhimu kujenga na kuboresha mazingira bora kwa wanafunzi ili waweze kujiinua kitaaluma.
Kutokana na hilo , Mwambashi aliwaelekeza ,watendaji wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo kuwa wazalendo,ili miradi hiyo itoe huduma katika jamii.
"Nimejiridhisha ,tumejiridhisha vizuri na kuona nyaraka za malipo, hivyo nazindua madarasa haya"alifafanua Mwambashi .
Wakati huo huo , Mwambashi aliwaasa wanafunzi kuacha matumizi mabaya ya TEHAMA kwa kuangalia vitu visivyo na maadili kwao.
Awali Mkuu wa wilaya ya Kibaha , Msafiri alibainisha ,walipata milioni 24 kutoka kwa wadau wa elimu ambapo milioni 7 walitenga na kununua madawati 50 ambayo yamegawanywa 25 Mji wa Kibaha na 25 mengine Kibaha Vijijini.
Mbio za mwenge pia zimekagua mradi wa shamba la mikorosho KJ 832 Ruvu ,lilianzishwa mwaka 2018 ,lina ukubwa wa hekari 115 na limegharimu milioni 36 .
Akielezea mradi huo,meneja wa shamba hilo ,Lugomola Kifusi anasema, kwa msimu huvuna tani 1.5.
Mwenge huo ukiwa wilayani Kibaha utakimbizwa katika miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 2.
No comments: