COSTECH YATAKA UCHUMI WA VIWANDA UENDANE NA KASI YA TEKNLOJIA



Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt.Amos Nungu akizunguma baada ya kufungua mkutano wa Mameneja 25 wa kumbi za bunifu kutoka mikoa mbali mbali nchini.
Mameneja wa kumbi za Bunifu kutoka mikoa mbali mbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dkt. Amos Nungu.
Mmoja wa Mameneja wa kumbi za ubunifu John Akanifute (Pwagu) ambaye anamiliki karakana ya umeme wa Maji mkoani Njombe akizungumza katika mkutano huo.


Na Karama Kenyunko Michuzi TV 

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt.Amos Nungu amesema uchumi wa viwanda unatakiwa uendane na kasi ya teknolojia iliyopo sasa, ambapo kampuni changa ndio zinakuja na teknolojia mpya tofauti na zile za zamani.

Dkt. Nungu ameyasema hayo leo Juni 30,2021 mkoani Dar es Salaam wakati  wa kikao cha mameneja 25 wa kumbi za ubunifu kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa bunifu.

Amesema kampuni changa zinamitaji midogo na hivyo wamalazimika kutumia Teknoloji toke wanapoanza kuingia sokoni huku kampuni za zamani tayari zikiwa zimekwisha seto na hivyo kubadilika kwenda hatua inayofuata, itachukua muda mrefu kwao kwani kuna usemi usemao  kama hakijakatika, hakijaaribika, kwa nini ukifanyie matengenezo?

Ameongeza kuwa, kama wabunifu wakiwa imara zaidi kwa ajili ya kuudumia jamii, basi uchumi wa viwanda ambao hutegemea ubunifu utafanikiwa  kwa hiyo watahakikisha na wao wanakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha hilo.

"Tanzania tuko uchumi wa kati wa chini tunakwenda uchumi wa kati wa juu, lakini uchumi wa viwanda tukianzia na ule mpango wa miaka mitano sasa hivi tunaongelea kutumia sayansi na teknolojia na ubunifu katika kuongeza tija," alisema Dkt. Nungu.

Alisema mwaka 2011 tume ilianzisha ukumbi wa ubunifu (Bun) kwa ajili ya kuwasaidia vijana wabunifu kukutana pamoja kubadilisha uzoefu kwani wanapo kutana wanakuwa na maarifa mbali mbali.

Dkt. Nungu amesema alisema, vijana wengi wakimaliza vyuo wanakuwa na ujuzi wa darasani lakini wakienda kwenye vitendo bado hawawezi, hivyo kukutana kwao kutawasaidi kujifunza kwa mapana zaidi.

"Vijana wengi kutoka vyuo vikuu vyetu wanatoka na maarifa yale ya darasani tu ,lakini hayo maarifa dunia unakuta hawana lakini kwenye hizi kumbi wanapata maarifa ya zaida hivyo wako hapa leo kubadirishana uzoefu, "

Aidha, alisema mameneja hao wapo waliyotoka vyuo vikuu, Chuo Kikuu Huria, Mzumbe, MUST, na taasisi za sekta binafsi ambapo wote wana Hub ambazo zinafanya kazi moja.

Mmoja wa mameneja hao, John Akanifute (Pwagu) ambae ana miliki karakana ya kusambaza maji mkoani Njombe, alisema ni vema teknolojia za ubunifu zikaamia kwa vijana kwa sababu umri wao unakwisha.

Akanifute alisema vijana wengi wamekuwa hawafanyi vizuri kwenye vitendo kwa sababu katika vyuo vingi , wanasoma zaidi kuliko kutenda kwa vitendo, lakini pale kwangu vijana wengi wanakuja kwa ajili ya kufanya mazoezi ya vitendo.

"Costech wameniwezesha kwa kunipa vifaa na wanataka kuniongezea vingine , kwa sababu natamani  karakana yangu iwe cliniki ya ubunifu kwa sisi ambao tumezoea kufanya kazi iwe pale  ili watu wa nyanda za juu kusini waje kujifunza," alisema

Naye, Japhet Sekenya, Muanzilishi wa Taasisi ya kumbu ya bunifu za kibaiolojia alisema , wao wamekuwa wakiwasaidia wabunifu kupeleka bunifu zao sokoni kwa kuwapa mafunzo kwa ajili ya ubunifu wa awali kisha kuwapatia vifaa wanavyohitaji ili waweze kufanya bunifu zao. 


No comments: