TUNZO ZA VIKOBA KUTOLEWA MWEZI AGOSTI 2021

Mwenyekiti wa Kamati ya Tunzo za Vikoba, Dkt. Amina Abdul (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Onomo Dar es salaam mwishoni mwa wiki, wakati wa kutangaza maandalizi ya Tunzo za Vikoba kwa vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa nchi nzima zinazoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Women Supporting Women. Tunzo hizo zinatazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti 2021. Kulia ni Yasinta Bokela ambaye ni Mwanachama Muasisi wa Tunzo hizo, Meneja Mauzo wa BankABC, Bertha Bash (wa pili kulia) pamoja na Meneja Masoko wa BankABC, Rose Ngowi.
Meneja Mauzo wa BankABC, Bertha Bash akizungumza na waandishi wa habari namna watakavyoweza kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Women Supporting Women kwenye Tunzo za Vikoba kwa vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa nchi nzima.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanachama wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Supporting Women ambao ni wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Tunzo za Vikoba kwa vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa nchi nzima.

No comments: