RC MONGELA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WATEULE
MKUU wa Mkoa wa Arusha Ndg .John Mongela amemuwapisha Mwl.Raymond Mwangwala ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro.
Kabla ya uteuzi huo Mwl.Raymond Mwangwala alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM.) Aidha Mongela amemuapisha Sophia Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
No comments: