RC MAKALLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA ZA DAR ES SALAAM
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla leo June 21, 2021 amewaapisha Wakuu wa Wilaya za Dar es Salaam baada ya kuteuliwa June 20, 2021 na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wakuu wa Wilaya wapya walioapishwa na RC Makalla ni Fatma Almasi Nyangassa (Kigamboni) na Kherry Denis James (Ubungo) wakati Jokate Urban Mwegelo (Temeke), Godwin Crydon Gondwe (Kinondoni) Ng’wilabuza Ndatwa Ludigija (Ilala) wakiendelea na majukumu yao ya awali.
Baada ya uapisho huo, Makalla amewataka Wakuu hao kufanya kazi kwa bidii katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu, amesema Rais anafahamu eneo kubwa la nchi ya Tanzania hivyo kuwa na imani nao katika nafasi hiyo ya uwakilishi wa Ukuu wa Wilaya.
“Nimefurahi kupata Wakuu wa Wilaya wapya, Kigamboni (Fatma Nyangasa) na Ubongo (Kherry James), naamini hawa wengine ni wazoefu katika majukumu yao hivyo natarajia mtafundishana kazi ili twende sawa”, amesema Makalla.
Amewataka Wakuu hao wa Wilaya kufika kwenye vituo vyao vya kazi na kutoa ushirikiano kwa Watendaji waliowatangulia katika vituo hivyo.
“Mkifika kwenye maeneo yenu ya kazi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii na ushirikiano, Rais amewaleta katika mkoa huu naamini ana matarajio na wote”, ameeleza Makalla.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo, Kherry James kwa niaba ya wenzake ameomba ushirikiano kwa sehemu walizopangiwa na Rais Samia Saluhu ili kufanikisha azma na matakwa ya Serikali ya Tanzania.
No comments: