Ongeza kipato chako: Kuwa dereva: masomo, gharama na vitu vya kujua.



Ikiwa unafikiria kuwa dereva wa Bolt, haya ni masomo na taarifa chache kuhusu gharama na vitu unavyohitaji kujua kabla ya kuanza.

Kuna faida nyingi za kuwa dereva wa Bolt. Unaweza kupata pesa wakati unataka, kuwa bosi wako wewe mwenyewe na una hiari maana hakuna ada ya kila mwezi unayohitaji kulipa!

Ikiwa unafikiria kuwa dereva wa Bolt, haya ni masomo na taarifa chache kuhusu gharama na vitu unavyohitaji kujua ili kuhakikisha kuwa unakuwa dereva wa Bolt kwa muda mrefu, wenye mafanikio na furaha!

Masomo ya udereva ili uanze

Kupata shule inayofaa ya udereva itakayokusaidia kujifunza jinsi ya kuendesha gari ni rahisi. Nenda kwenye mtandao na uandike "shule za kuendesha gari zilizo karibu" na utapata orodha ya shule hizo.

Gharama ya masomo ya udereva kwa ujumla ni nafuu sana na thamani ya ustadi utakaoupata ni kama dhahabu, maana itakuongezea ustadi wa juu wa usalama barabarani na fursa za kupokea takrima zaidi kutoka kwa wateja wako wenye furaha.

Tafadhali jua kwamba unahitaji kuwa na leseni halali ya udereva kabla ya kujisajili kama dereva wa Bolt nchini Tanzania.

Jiandikishe na ufanye biashara.

Huku tukifanya bidii kuhakikisha kuwa kila wakati tunapata washirika wanaofaa, kusajiliwa kwa dereva wa Bolt ni mchakato rahisi, ulioboreshwa.

Fomu yetu ya usajili wa udereva inakuchukua dakika 5 tu kukamilisha na kuwasilisha. Mara tu unapokubaliwa na kusajiliwa kama dereva, utahitaji kumaliza mafunzo yako ya udereva ama katika ofisi ya Bolt au mtandaoni.

Tutapitia nyaraka zinazohitajika na mara tu tutakapokamilisha, tutakufungulia akaunti ya dereva katika programu ya Dereva wa Bolt. Utahitaji kuwa na simu janja ‘smartphone’ inayofanya kazi ambayo angalau inatumia mfumo wa Android 9.0 au iOS 12, ili uweze kuchukua abiria na kuwafikisha mwisho wa safari yao.

Ikiwa huna simu mahiri, timu yetu inaweza kupendekeza simu ya bei nafuu ya Android ili uanze.

Weka gari yako katika hali nzuri.

Ikiwa tayari una gari, utahitaji kuifanya ionekane jinsi ilivyokuwa wakati ulipoinunua kutoka kwenye chumba cha maonyesho ya magari.

Moja ya vitu waendeshaji wa Bolt hutegemea katika ukadiriaji wao ni hali ya mambo ya ndani ya gari lako. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa ni safi iwezekanavyo. Utahitaji kuwekeza katika usafishaji wa viti ikiwa havijasafishwa kwa muda mrefu na hakikisha kuondoa madoa yoyote na harufu mbaya.

Kumbuka kwamba uboreshaji mwingine wa mfumo wa hewa unaweza kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo uwe makini kabla ya kununua air freshener.

Je! Unafanyaje ikiwa hauna gari au gari lako halikidhi vigezo vya Bolt kwa safari inayokubalika?

Bolt inaweza kukusaidia kupata gari kutoka kwenye orodha ya magari yetu au kutoka kwa washirika wetu wenye huduma ya kukodisha ikiwa hauna gari linalofaa. Kuna anuwai ya gari mpya na zilizotumiwa kwa kuendesha kama mshirika wa Bolt. Unaweza kuchagua kukodisha gari kwa muda mfupi au mrefu kwa muda usiojulikana, kwa kiwango cha bei nafuu.

Ongeza kiwago chako cha kujichanganya na kijamii.

Hata kama wewe ni mpole, hiyo haimaanishi kuwa huwezi kuwa dereva mzuri. Ila, ni muhimu kukumbuka kuwa ingawa shughuli yako kuu ni udereva, bado uko kwenye biashara ya huduma kwa wateja.

Moja ya mambo muhimu zaidi unayoweza kufanya katika kila mwingiliano ni kuanzisha mazungumzo na abiria wako yanayolenga kuzuia kutokuelewana. Ni muhimu kuzingatia kwamba viwango vya chini vya udereva vinaweza kumaanisha kupoteza sifa za udereva na kufutwa kwenye mfumo ya Bolt.

Hakikisha kumsalimia abiria wako mara tu wanapoingia kwenye gari lako. Kuwa karibu zaidi na jamii, inaleta matokeo mazuri!

Hapa kuna zana za mazungumzo 101 ambazo unaweza kutumia kwenye safari yako ya Bolt ijayo.

Jaribu kufahamu kwamba wakati abiria wengine watafurahi zaidi kuwa na mazungumzo, wengine wanataka tu kupotea katika mawazo yao wakati wanaangalia ulimwengu ukipita. Jihadhari na baada ya muda mfupi utakuwa mtaalamu wa kusoma abiria wako ili uweze kupima kama wako kwenye hali ya gumzo au la.

Ikiwa unaendesha gari katika eneo lenye watalii wengi, inaweza kusaidia kujifunza misingi ya lugha chache na maneno ya kawaida ili kupunguza kizuizi cha mawasiliano. Kwa kuongezea, mwishoni mwa safari, hakikisha kumuaga abiria wako na kuwatakia mapumziko mema ya siku yao, ili uweze kuwa na hakika ya kuacha maoni mazuri ya kudumu kwa abiria.

Jihadhari mwenyewe

Kupata pesa kama dereva wa Bolt inaweza kuwa zoezi ya kufurahisha, lakini pia inaweza kuwa kazi ngumu, kwani inahitaji kutumia muda mwingi kukaa chini, wakati mwingine katika hali zenye mkazo ikiwa uko kwenye foleni ndefu, ukiendesha kwenye eneo mkanganyiko au una abiria aliechelewa safari yake kama kupanda ndege.

Kwa sababu hii, ni muhimu sana kutunza afya yako ya mwili na akili.

Hakikisha kuchukua mapumziko ya mara kwa mara wakati wa kuendesha gari ili uweze kutoka na kunyoosha miguu yako. Kunya maji mara kwa mara, kula kiafya na upate usingizi mzuri wa hali ya juu ili ubaki makini na uwe umepumzika vizuri ukirudi barabarani.

Kwa kuongezea, wakati inaweza kuvutia kufanya kazi kadri uwezavyo ili kuongeza mapato yako, hakikisha kuchukua muda wako na watu unaowapenda. Hii itahakikisha wakati wako wa kuendesha gari na Bolt ni mrefu, wenye furaha na ustawi!

Je, una kile kinachohitajika kufanikiwa kama dereva wa Bolt? Anza leo!

No comments: