NAIBU WAZIRI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDAAJI MASHINDANO YA UREMBO AFRIKA MASHARIKI
mazungumzo yakiendelea. |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma.
Waandaaji hao ni bi Jolly Mutesi ambaye ni makamu wa Rais anayetokea nchini Rwanda na bi Mariam Ikoa ambaye ni muandaaji wa kimataifa anayetokea Tanzania.
Katika mazungumzo hayo na waandaaji hao wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk amewapongeza waandaaji hao kwa kuja na wazo hilo pamoja na kutaka kufahamu miongozo na itifaki za kufuatilia ili kufanikisha mashindano hayo.
Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa mashindanoo hayo Bi Mariam Ikoa amemuelezea Mhe. Naibu Waziri Mbarouk kwamba ujio wao Wizarani una lengo la kujitambulisha pamoja na kupata miongozo na itifaki za jinsi ya kuendelea na taratibu za mashindano hayo ya urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Amesema mashindano hayo yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 20, 2021.
No comments: