KITUO CHA ELIMU YA AFYA KWA NJIA YA MASAFA CHAZINDULIZIWA MOROGORO

 Morogoro. Kituo cha elimu kwa njia ya masafa (CDE) na mfumo wa e-Learning kimezindulikwa ili kuendelea kuratibu mafunzo ya kujiendeleza kwa watumishi wa sekta ya afya wakiwa makazini kama sehemu ya kuboresha stadi za kazi, kuongeza ujuzi na umahili katika kutekeleza majukumu yao ya kitaaluma mkoani hapa.

Akizungumza baada ya kuzindua mfumo huo na kukabidhi mkoani hapa, Kaimu katibu mkuu wizara ya afya,  Dk Loishook Saitore Lazier alisema kuwa dunia inabadilika kutokana na kukua kwa teknolojia kila kukicha.

Dk Lazier alisema kuwa miaka ya 1970 hadi 1980 dunia imekuwa na mabadiliko mengi, kama sekta ya afya maeneo ya mafunzo na kuongeza ujuzi hawapendi kuachwa nyuma na dunia mzima inajifunza mambo mengi kwa njia ya masafa na eletroniki.

“Serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia na watoto imeandaa na kukamilisha maandalizi ya mfumo wa kujifunzia kwa njia ya elektoriniki kwa watumishi waliopo makazini kupitia wadau mbalimbali.”alisema Dk Lazier.

Ukamilishwaji wa mfumo huu katika ngazi zote uliratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation chini ya uongozi wa Wizara ya Afya na ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) kwa kujumuisha pia wadau mbalimbali ambao ni Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mabaraza ya Taaluma za Afya, Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), Tanzanian Training Centre for International Health (TTCIH).

Utengenezwaji wa mfumo huu mpaka katika hatua hii umegharimu shilingi za kitanzania 450,101,010 na mpaka sasa mfumo huu umeweza kudahili na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 34, 357 na watumishi wa Afya 11,507 waliopo kazini wamendelea kupokea mafunzo kupitia mfumo huu katika kozi mbali mbali.

Dk Lazier alisema kuwa amewaomba kufahamu kuwa kukabidhiwa mfumo ni kitu kimoja lakini kuutumia mfumo kwa manufaa yao ni jambo lingine hivyo mfumo huo utumike kama kifuta machozi, kama jawabu kwa kutumika kama fursa muhimu kwa manufaa katika fani ya afya.’alisema Dk Lazier.

Dk Lazier ameyaomba mabaraza ya kitaaluma na vyama vya kitaaluma kwa hiyo ni fursa ambayo walikuwa wakiitamani miaka mingi sasa tayari mfumo una fanya kazi.

“Nitoe rai kwa watumishi waliopo kazini wamekuwa na mazoea ya kuwa wakimaliza shule, vitabu wanafunika na kuweka pembeni sasa kabla ya mtumishi hajahuuisha leseni yake anatakiwa kuonyesha amejiendeleza kwa namna gani ili kupata leseni nyingine.”alisema Dk Lazier.

Dk Lazier alisema kuwa lengo la kuwataka watumishi wa afya kujiendeleza sio jambo geni kwani binadamu wana tabia za kumbukumbu kupotea, kusahau na katika taalumu ya afya na matibabu kusahau sio jambo jema sana kwa sababu kile unachosaahau kinahitajika katika kuokoa maisha ya mgonjwa siku moja.

Mkuu wa chuo cha afya na sayansi shirikishi Morogoro, Ndementria Vermand alisema kuwa mafunzo kwa njia ya masafafa imelenga kutoa huduma bora za afya kwa walengwa katika kutoa elimu za masafa kwa watumishi wa afya ili kuboresha stadi za kazi, kuongeza ujuzi na umahili katika kutekeleza majukumu yao ya kitaalumua.

Vermand alisema kuwa watatumia mbinu mchanganyiko na jumuishi za vipindi vya ana kwa ana, kujisomea na kufanya mazoezi ya vitendo kwa wanafunzi ikiwa ni mkakati mkubwa wa kukabiliana na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.

Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo na maendeleo ya wataalamu wizara afya, Dk Fadhil Lyimo alisema kuwa uzinduzi na makabidhiano ya mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao limekuwa tukio la kihistoria katika mapinduzi ya mfumo wa kufundisha na kujifunza kwa watumishi wa afya nchini.

Dk Fadhil Lyimo alisema kuwa wanalo jukumu la kubuni njia mbalimbali kuhakikisha watumishi wa sekta ya afya wanaendelezwa bila kuathiri utoaji wa huduma katika vituo vyao vya kazi.


Kaimu katibu mkuu wizara ya afya,  Dkt Loishook Saitore Lazier kushoto na Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo na maendeleo ya wataalamu wizara afya, Dk Fadhil Lyimo (Katikati) wakimsikiliza Mtaalamu wa mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao, Ashraf Mdhakiru wakati wa makabidhiano na uzinduzi wa kituo cha elimu kwa njia ya masafa (CDE) na mfumo wa e-Learning Morogoro.


Kaimu katibu mkuu wizara ya afya,  Dkt Loishook Saitore Lazier akibonyeza kitufe katika kompyuta wakati wa makabidhiano na uzinduzi wa kituo cha elimu kwa njia ya masafa (CDE) na mfumo wa e-Learning Morogoro, mwenye Kaunda suti nyeusi ni Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo na maendeleo ya wataalamu wizara afya, Dk Fadhil Lyimo (Katikati) wakimsikiliza Mtaalamu wa mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao, Ashraf Mdhakiru

 

No comments: