JAFO AZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Charles James, Michuzi TV

SIKU Moja kabla ya kilele Cha Siku ya Mazingira duniani, Serikali imezindua Mpango mkakati wa Taifa wa kukabidhiwa na mabadiliko ya tabia Nchi mwaka 2021 hadi 2026.

Mpango huo umezinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo leo jijini Dodoma ambapo amewataka wananchi kuishi kwa kufuata misingi ya ajenda za kimazingira.

Katika uzinduzi wa Mpango huo, Waziri Jafo pia amefungua kongamano la hifadhi ya mazingira na maendeleo endelevu na kusema kuwa mkakati huo utasaidia kuondokana na uharibifu wa mazingira.

" Kutokana na mapinduzi ya viwanda na shughuli za kibinadamu kumechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya Tabia Nchi na kuipa changamoto Dunia katika kutafuta suluhu za kimazingira.

Ndugu zangu jukumu la kulinda mazingira ni letu sote, bila kulinda mazingira hapa duniani siyo sehemu salama hivyo kuna kuna haja kwa Nchi zilizoendelea kusaidia Nchi maskini kupamban na athari za kimazingira zinazosababishwa na tabia nchi," Amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema zaidi ya watu Milioni 1.6 wa Ukanda wa Pwani watakabiliwa na changamoto za kimazingira ifikapo mwaka 2030 endapo jamii itaendelea na shughuli zake zinazoathiri mazingira.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la CARE International Tanzania, Haika Mtui ameipongeza Wizara ya Mazingira kwa namna inavyoendesha mapambano yake dhidi ya uharibifu wa mazingira huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akikabidhi Mpango mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi kwa wadau mbalimbali wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira waliohudhuria uzinduzi wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabia Nchi.

No comments: