SHULE YA ST.JUDE INATAKIWA KUUNGWA MKONO KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA YA KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-MBUNGE GAMBO
Na Jusline Marco-Arusha
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo amesema kuwa Shule ya St.Jude inatakiwa kuungwa mkono kutokana na kazi wanayoifanya ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu bure jambo ambalo sehemu ya utelelezaji wa sera ya serikali ya elimu bure ambayo walishaanza kuitekeleza muda mrefu na kwa upana zaidi.
Akiwa katika ziara yake ya siku moja iliyofanyika Shuleni hapo amejiridhisha na huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na namna wanavyoendesha mchakato mzima wa upatikanaji wa watoto kwa kuishirikisha serikali ya mtaa na kijiji ambapo amesema kutokana na changamoto zilizoibuka hivi baada ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuifungiaakaunti ya shule hiyo na kuchukuwa kiasi cha fedha kolichopo kwenye akaunti hiyo sholingi milioni 500,ameahidi kuzungumza na wizara husika juu ya jambo hilo.
"Fedha hizo zilizochukuliwa nimeambiwa zilikuwa za mahitaji ya shule ikiwemo mishara ya wafanyakazi, chakula na malazi mengine ya wanafunzi hawa jambo ambalo nimeshaongea na waziri mwenye dhamana na ameniahidi atalishughulikia ili muweze kuendelea na kazi yenu hii ya kuisaidia serikali kutoa elimu bure ma hamfanyi biashara sasa mkiambiwa mlipe kodi fedha hizo zitatoka wapi?,"Alieleza Gambo.
Alifafanua kuwa katika suala la vibali vya kazi kwa wafanyakazi wakigeni wawili hilo nalo atazungumza na wanaohusika ili kuangalia ni namna gani wanawasaidia kuendelea kufanya kazi kwa amani ambapo shule hiyo ina wafanyakazi 302, 297 wakiwa ni watanzania sawa na asilimia 97, huku watano wakiwa ni wageni sawa na asilimia 3 jambo ambalo endapo shule hiyo itafungwa watakaoumia ni wazawa.
Alisema kuwa shule hiyo haijiendeshi kibiashara ambapo ina wanafunzi zaidi ya 1800, 437 wakiwa ni wa shule ya msingi, sekondari ya wasichana yenye mchepuo wa sayansi 428 na waliobaki wakiwa ni wanafunzi wa shule mchanganyiko iliyopo Usariver ambao ni kwanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita huku wote wakipata elimu kwa ufadhili wa watu wa Australia.
"Serikali yetu inatoa elimu bure kwanzia chekechea hadi kidato cha nne lakini tunawaona hawa wanatoa bure hadi kidato cha sita kwakeli serikali inatakiwa kuwaangali na kuweza kuwaondolea hizi changamoto kwani tunatamani shule hii ikue na kuenea Tanzania bara yote na kufika Tanzania visiwani pia, kwani hata kule kuna watoto wanaoishi katika mazingira magumu,"Alisema Gambo.
"Kazi wanayoifanya St Jude ni kazi ya Mungu na sio ya kidunia na wanaishirikisha serikali kwa asilimia 100, wamekubali kutoka kwenye nchi zao na kuja kuweka alama ya kuondoa umasikini Tanzania kwa kuwafadhili watoto wetu wanaishi katika mazingira magumu kupata elimu ya msingi hadi sekondari ya juu bure, watu kama hawa wanatakiwa waitwe na kuulizwa wanapokwama na kusaidiwa ili waweze kuendelee kuzalisha matunda katika nchi yetu,"Alisisitiza Gambo.
Kwa upande wao viongozi wa wanafunzi upande wa shule ya msingi Johnson Eliasafu na ipande wa shule ya sekondari ya wasichana Vivian Gasper walisema kuwa ziara hiyo imekuwa taa ya matumaini ya uhusiano mzuri kati yao, jamii na serikali kwa ujumla ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Waliongeza kuwa pamoja na changamoto mbalimbali,wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakishiriki maonyesho ya ugunduzi wa kisayansi, ambayo hufanyika kila mwaka katika shule ya sekondari ya St.Jude ambapo miradi yao imekuwa ikipata alama nzuri ikiwa ni uungaji mkono juhudi za serikali za kuzalisha wataalamu wa masuala ya kisayansi.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bibiana Mardai alisema kuwa wanaiomba serikali iangalie shule hiyo kwa jicho la pili kwani wanawasaidia watoto wa Kitanzania ambao pengine wangeshindwa kusoma kutoka kana na hali duni za familia zao kuweza kufikia maono ya na ndoto zao kwa kupata elimu ambayo itawasaidia kuja kuzitumikia jamii zao hapo baadae.
Vivian GasperDada Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya St.Jude akisoma risala yao mbele ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo wakati alipotembelea shule hizo ili kujiridhisha na huduma zitolewazo kwa wanafunzi hao.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo akipata maelezo mafupi kutoka kwa mwalimu wa Fizikia wakati alipotembelea maabara ya Fizikia,Kemia na Baiolojia katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya St Jude iliyopo Mkoani Arusha.
No comments: