MBUNGE WA ARUSHA MJINI ATEMBELEA SHULE YA ST JUDE KUJUA CHANGAMOTO ZAO.
Jana tulitembelea Shule ya ST Jude Jijini Arusha ili kujua changamoto zao. Shule hii ni Baraka kwa Jiji letu na Watoto wa Taifa letu maana inasomesha Watoto kutoka kwenye Familia masikini na Wenye mazingira magumu.
Shule hii inaendeshwa kwa michango na misaada ya wafadhili kutoka Australia na Nchi nyingine duniani. Kwenye shule hii Watoto wanapata bure Elimu, Chakula, Sare za Shule, usafiri na mengineyo. Wanaunga mkono sera ya Serikali ya Awamu ya 6 ya Elimu bure ikiwa ni pamoja na kusomesha Watoto 600 wa kike kila mwaka. Shule hii ina watoto zaidi ya 1800 na imetoa ajira 302.
Bodi ya Shule imeomba Serikali isaidie yafuatayo:-
1. Isamehewe kodi kwa kuwa hakuna Mwanafunzi anayelipa chochote na wafadhili wamesamehewa kodi na kwenye nchi zao ili kusaidia watoto wa Tanzania. TRA walifunga akaunti ya Shule hii na kuchukua Million 500 Nov 2020 za watoto hawa masikini.
2. Wapate Vibali vya kazi vya “Fundraising Manager” na Marketing manager” ambayo ni rahisi kuwashawishi wafadhili maana kwenye misaada watu wa nje wanaaminiana wenyewe kirahisi.
Ni imani yangu kuwa Mungu ataweka mkono wake ili shule hii iendelee kuwa Baraka kwa Watoto wa Jiji letu na nchi yetu!
No comments: