Mashabiki wawili wa soka washinda Sh145.9m za M-BET
Mashabiki wawili wa soka Tanzania wamejishindia jumla ya Sh145, 957, 650 baada ya kubashiri kiusahihi zaidi jumla ya mechi 12 katika mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 wa kampuni ya michezo ya kubah M-Bet Tanzania.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi amewataja washindi hao kuwa ni Juma Makongo ambaye ni mkazi wa Mwananyamala, Dar es Salaam na Juma Mussa Ngua kutoka mkoa wa Singida.
Mushi alisema kuwa washindi hao wametumia Sh1,000 tu kubashiri mechi hizo 12 za ligi mbalimbali hapa duniani na kuweza kugawana kiasi cha fedha hicho.
Alisema kuwa Makongo na Ngua wanakuwa washindi wa nane tokea kuanza kwa mwaka na kampuni yao imetumia zaidi ya Sh milioni 550 kuwazawadia washindi mbalimbali walioweza kubashiri kwa usahihi na kuibuka washindi.
“Tunafuraha kuwazawadia washindi hawa na tunaamini kuwa wataweza kubadili maisha yao kupitia fedha walizoshinda. M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa,” alisema Mushi.
Akizungumza baada ya ushindi huo, Ngua ambaye ni shabiki wa Simba alisema kuwa hakuamini kupata kiasi kikubwa cha fedha hicho ambacho atasaidia wazazi wake na kuanzisha biashara.
“Mimi ni mmachinga, sikutegemea kupata kiasi kikubwa cha fedha hiki na nitaanza kujenga nyumba kwa wazazi wangu huku nikiboresha biashara,” alisema Ngua.
Mkuu wa Kitengo cha Michezo ya kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga aliipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri hapa nchini.
Mwanga alisema kuwa michezo ya kubahatisha inachangia kwa kiasi kikubwa sana pato la taifa.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-bet Tanzania, Allen Mushi (Katikati) akizungumza wakati wa kutangaza washindi wawili wa mchezo wa Perfect 12.Kulia ni mmoja wa washindi, Juma Ngua na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Michezo ya kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga
Meneja Masoko wa kampuni ya M-bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa mchezo wa Perfecr 12, Juma Ngua(Katikati). Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Michezo ya kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga.
No comments: