Ecobank Tanzania yazindua mpango maalumu wa kuwainua Wanawake

 

ECOBANK Tanzania imezundua rasmi mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ wenye lengo la kuwasaidia na kuwainua Wanawake Wajasiriamali katika masuala mbalimbali ya kifedha na kuwaongezea kipato ili waweze kumudu biashara hizo na kupata mafanikio.


Mpango huo ni maalum kwa Benki hiyo kuwaelimisha Wanawake hao jinsi ya kufanya biashara hizo sambamba na kuwapa mikopo kwa bei nafuu. Ili kuwa na vigezo ni lazima Wanawake hao Wajasiriamali wawe na Leseni za Biashara na kufungua Akaunti katika Benki hiyo.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Charles Asiedu amesema mpango huo ni maalum ambao utawaidia wanawake wajasiriamali kuongeza mtaji wao na kupata faida.


Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa amesema mpango huo ni fursa kwa Wanawake wajasiriamali hivyo ametoa wito kwa Wanawake hao kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Benki hiyo.

Bi. Beng’I amesema fursa hiyo itawapa Wanawake hao maendeleo ya kijamii na Kiuchumi hivyo kupelekea idadi kubwa ya ajira kwa vizazi vijavyo katika nyanja hizo hususan katika biashara.

Ecobank Tanzania yazindua mpango maalumu wa kuwainua Wanawake

No comments: