WASHINDI WA TUZO ZA MALKIA WA NGUVU 2021 WAWASHUKURU CLOUDS MEDIA

  Na Avila Kakingo- Michuzi TV

WASHINDI wa Tuzo za Malkia wa Nguvu zilizoandaliwa na Clouds Media Group wawashukuru waandaaji wa tuzo hizo.

Wakizungumza mara baada ya kutunukiwa tuzo katika kila sekta iliyopangwa leo Aprili 24, 2021 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere katika tuzo za Malkia wa nguvu 2021.

Mshindi wa tuzo ya kilimo biashara, Rose Swai amewashukuru Clouse Media huki akiwaahidi kutengeneza kabati la kiyoo kwaajili ya kuihifadhi tuzo aliyoishinda kwaajili ya kuonyesha vijana na watu wengine wanaotaka kujifunza.

Pia amewaombe Clouds Media waweze kudumu ili waweze kuwapata Malkia wa nguvu wengi zaidi kwaajili ya Maendeleo ya taifa.

Rose ni mwanamke mwenye miaka 71 anayejishughulisha na biashara ya utengenezaji kahawa..

Hata hivyo Mshindi wa tuzo ya Sekta ya Michezo Innocensia Masawe amewashukuru Clouds Media group huku akiwaomba wadau wa michezo kumuunga mkono katika juhudi za kuinua vipaji vya wachezaji pamoja na kusaidia kuiendelea timu yake ya  Mpira wa miguu iliyopo mkoani Dodoma.

Licha ya hilo Mshindi katika tuzo ya Sekta ya Afya na Ustawi wa jamii, Profesa Paulina Mella amewashukuru Clouds Media Group na kusema kuwa "Ni miaka mingi nimeanzisha degree ya maafisa uuguzi na sasa nimeshastaafu."

Nawashukuru wanafamilia yangu, hasa Mume wangu kwa kuniruhusu kwenda kusoma, nilimwachia watoto wangu wadogo ili nikasome." Amesema Prof. Paulina.





 

No comments: