TUZO ZA MALKIA WA NGUVU 2021, TUZO YA HESHIMA YALIZA WENGI

   Na Avila Kakingo- Michuzi TV

TUZO ya heshima imekuna watu wengi kwani ilipokuwa ikioneshwa makala ya Mtunukiwa kila mtu aliinama na kuisikiliza, huku wakitazama kwa macho yenye unyevunyevu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo katika jiji la Ilala Mkoa aa Dar es Salaam palipofanyika tuzo za malkia wa nguvu 2021 zilizoandaliwa na Clouds Media Group.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo leo Aprili 24, 2021,  Consola Eliya amesema kuwa tuzo hiyo ni kwaajili ya watanzania wote kwani anaishi na watoto zaidi ya 50.

Amesema kuwa watoto anao ishinao nyumbani kwake ni kwa msaada wa wa Mungu na aliwiwa kulea watoto kutokana na maisha aliyoyaishi.

Kwa maisha aliyosimulia kwenye Makala yake  tuzo hiyo anastahili kwani familia aliyoamua kuihudumia kwa miaka kadhaa ambayo amejaliwa.

Waliopata tuzo hizo kulingana na vipengele vilivyopangwa ni pamoja na
Tuzo ya heshima ametunukiwa Consola Eliya, tuzo, katika sekta ya afya aliyetunukiwa tuzo hiyo ni Paulina Mella huku tuzo ya biashara ya Chakula akiwa  ametunukiwa Neema Kasava.

Tuzo ya kiwanda cha burudani ametunikiwa Seven Mosha huku tuzo ya Mhamasishaji ikinyakuliwa na Herrieth Mkangaa ambaye anakauli mbiu ya kuishi kwaajili ya watu wengine na ameweza kuokoa zaidi ya wanawake changudoa zaidi ya 100 Mkoani Morogoro.

Wakati huo huo tuzo katika sekta ya Kilimo na Biashara tuzo hiyo ilinyakuliwa na Rose Swai, tuzo katika sekta ya Michezo ilinyakuliwa na Innoncensia Masawe ,
 ambaye ni miliki wa timu ya Mpira wa Miguu mkoani Dodoma  na tuzo katika sekta ya Mitindo na Urembo ametunukiwa na Mama Jadore.

Tuzo zingine ni katika sekta ya Sayansi na Teknolojia iliyonyakuliwa na Lilian Mkoi, pamoja na tuzo ya malkia wa nguvu ajaye ametunukiwa Getrude Mligo.

Kauli mbiu mwaka huu ni ya tuzo za malkia wa nguvu ni " Malkia wa nguvu 2021 ingia Ulingoni." ikiwa na maana ni kushindania.











 

No comments: