Wanawake Mloganzila wafanya usafi wa mazigira
.Baadhi ya watumishi wanawake wa MNH-Mloganzila wakifanya usafi katika mazingira ya nje ya hospitali ikiwa ni kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (kushoto) akiongoza zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika leo hospitalini hapa.
Wafanyakazi wanawake wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamefanya usafi wa mazingira ya nje ya hospitali ikiwa sehemu ya shughuli za kijamii na kujitolea katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili–Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema lengo ni kuimarisha usafi wa mazingira hasa katika maeneo yote yanayozunguka hospitali .
“Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali tumeshirikiana kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hospitali yetu ili wateja wetu wanaofika kupata huduma wawe katika mazingira safi na salama” amesema Dkt. Magandi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUGHE Tawi la Mloganzila Bi. Sperancia Mhapa ameishukuru uongozi wa hospitali pamoja na wanawake wote waliojitokeza na kufanikisha zoezi la kufanya usafi na kuahidi kuwa watahakikisha shughuli za kijamii zinakua endelevu.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mwaka huu ni “Wanawake katika uongozi ni chachu kufikia Dunia yenye usawa”.
No comments: