UWEPO WA CHUKI,MAJUNGU KWA WANAJAMII DHIDI YA WANAWAKE NI MIONGONI MWA VIKWAZO VYA KUTOFIKIA MALENGO-TAMWA ZANZIBAR
Muhammed Khamis,TAMWA-Zanzibar
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa amesema uwepo wa chuki na majungu kwa wanajami dhidi ya wanawake ni miongoni mwa vikwazo vikubwa vinavyowakwamisha wanawake wengi kutofikia malengo yao yakiwemo kushika nafasi mbali mbali za uongozi.
Dkt,Mzuri ameyasema hayo wakati alipokua akitoa mada kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake Duniani yaliofanyika ukumbiwa wa Sheikh Idrisaa Abdulwakil kikwajuni mjini hapa.
Alisema Zanzibar imejaliwa kuwa na wanawake wengi wenye uwezo mkubwa wa kushika nafashika nafasi za uongozi na nyenginezo kwenye jamii zao lakini wamekua wakishindwa kufanya hivyo kufuatia majungu na fitina wanazopikiwa dhidi yao.
Alieleza kuwa kutokana na mazingira ya aina ni wazi kuwa wanawake wengi hushindwa kutimiza ndoto hizo na kubaki kuwa wasindikizaji licha ya kuwa wao ndio idadi kubwa zaidi kuliko wanaume kwa mujibu wa takwimu za uandikishaji wapiga kura.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo alisema licha ya uwepo wa chanagmoto hizo lakini taasisi mbali mbali zimeweza kufanya kazi zake ikiwemo kuwahamasisha wanawake kujitokeza na hufanya hivyo.
‘’Kwa mfano mdogo tumeona uchaguzi mkuu uliopita wanawake watano walijitokeza kuwania kuteuliwa na chama cha CCM tena kwa nafasi kubwa ya Urais lakini haikua bahati kwao’’aliongezea.
Sambamba na hayo aliwataka wanawake kutoakata tamaa badala yake wawekeze nguvu zaidi mapema katika mipango yao ikiwemo ya kushika nafasi za uongizi.
Katika hatua nyengine aliwataka wanawake na jamii kwa ujumla kuazia sasa kuchana na msamiati kuwa mwanamke akiwezeshwa anaweza badala yake wanapaswa kufahamu kuwa mwanamke si mtu anaehitaji kuwezeshwa kutimiza malengo yake bali ni haki yake ya msingi.
Aidha aliwataka wanawake wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kufahamu kuwa rafiki wa mwanamke ni mwanamke mwenzake hivyo kupitia mtazamo huo wanawake hawapaswi kubaguana bali wapendane kwenye kila jambo.
Awali akifungua kongamano hilo Makamu wa Rais Zanzibar Hemed Sleiman Abdalla alisema wanawake ni watu muhimu na wenye uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu yao.
Alieleza kuwa wao kama Serikali wanatambua na wataendelea kutambua umuhimu wa wanawake na ndio maana wamekua wakiwapa nafasi kubwa kwenye uteuzi.
‘’Kwa mfano bado nafasi za wakurugenzi wa taaisisi mbali mbali za Serikali tutahakikisha tunawekeza nguvu zetu zaidi kwa wanawake kutokana na uchapaji wao wa kazi wanapopewa majukuku’’aliongezea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika kila ifakapo tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka na hubeba ujumbe mahsusi ambao unalenga kuwainua wanawake katika haki zao za msingi.
No comments: