KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWAZAWADIA MAFUTA WANAWAKE MASHUHURI, WAJASIRIAMALI
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania ambayo ni namba moja katika biashara ya mafuta imeungana imeungana na wanawake wote duniania katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mwanamke inayo adhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka huku ikieleza kwamba inatambua na kuthamini mchango wa makundi yote ya wanawake nchini katika kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu.
Aidha kampuni hiyo kwa kutambua umuhimu wa siku ya Wanawake Duniani , pamoja na mchango wao imeamua kuitumia siku ya leo pamoja na mambo mengine kutoa zawadi ya mafuta kwa wanawake katika makundi mbalimbali wakiwemo wanawake viongozi, mashuhuri pamoja na wanawake wajasiriamali wadogowadogo walioko kwenye maeneo mbalimbali.
Wakizungumza wakati wa kuadhimisha siku hiyo na baada ya kutoa zawadi ya mafuta kwa wanawake wa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake wanaondesha Bajaji kwa ajili ya kujitafutia riziki, maofisa wa kampuni kwa nyakati tofauti wameeleza kwamba kwa kutambua umuhimu wa Wanawake kwenye jamii ya kitanzania na wakiwa msatari wa mbele kusheherekea mafanikio ya wanawake walioko nchini, kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited imeamua kuadhimisha siku hiyo kwa kuwatambua baadhi ya wanawake wa kupigiwa mfano kwenye jamii yetu na kuwazawadia full tank ya mafuta kwenye magari yao pamoja bajaji.
Akielezea zaidi baada ya kuwazawadia mafuta wanawake hao wakupigiwa mfano iliyo fanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Upanga, Meneja wa Operations wa Kampuni Lameck Hiliyai amesisitizia Puma Energy Tanzania inathamini mchango wa wanawake katika kampuni na katika jamii na inafanya kila jitihada kuhakikisha kunakuwa na uwiano unaoridhisha wa wanawake na wanaume katika kampuni.
Aidha, amewahamasisha wanawake kujitokeza zaidi kushiriki katika shughuli mbalimbali katika biashara ya mafuta na kuachana na kasumba zilizo zoeleka kwamba hizi ni shughuli za wanaume na kwamba kampuni hiyo ambayo ni namba moja Tanzania katika biashara ya mafuta ni wajibu wao kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi wao wanawake lakini zaidi wanawake katika jamii mbalimbali zinazowazunguka.
Awali Meneja wa Rasilimali watu wa Puma Energy kwa bara Afrika Loveness Hoyange alieleza kuwa kampuni hiyo inatambua namna wanawake hao wanavyocharika katika harakati za ujenzi wa taifa. "Tunatambua namna gani wanawake siku hizi wanajituma, mfano hawa wenye ulemavu hawajachukulia hali yao kuwa sababu ya kujibweteka wanafanya kazi inayowawezesha kuendesha maisha".
Ameongeza kwa kuliona hilo, kampuni yao imeamua kuwapatia mafuta ili nao waweze kusherehekea siku hii ya wanawake kwa pamoja huku akisisitiza wanatambua mchango wao katika sekta ya usafirishaji.
Kwa upande wake mwanamama Jasimin Milanzi mwenye ulemavu wa viungo ambaye anajishughulisha na utoaji huduma ya kusafirisha abiria kwa kutumia usafiri wa bajaji, amesema anajisikia fahari kuwa miongoni mwa wanawake ambao wamepata zawadi ya kujaziwa mafuta na kampuni hiyo na imedhihirisha kumbe nao mchango wao kwenye jamii unatambulika huku akisisitiza licha ya kwamba ni walemavu wa viungo lakini wana akili kama walivyo binadamu wengine.
No comments: