MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AZINDUA MRADI WA AMKA MWANANGU SOMA KWA BIDII
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii wa Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Mshika Fedha wa Taasisi hiyo Bi, Valeria Rashid Haroub, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar jana usiku 7-3-2021.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wabunge na Viongozi wa mbalimba na Wananchi wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, wakati Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuuzindua Mradi huo jana usiku 7-3-2021, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Risala ya Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) na Katibu wa Jumuiya hiyo Bi. Tatu Hussein Abdalla, wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar jana usiku 7-3-2021.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akihutubia na kuzindua Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, mradi huo wa Jumuiya ya Rafiki wa Mwanamke na Watoto Zanzibar.(RAWWAZA) uzinduzi huo umafanyika jana usiki 7-3-2021 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Bi. Suzan Kunambi na Mwenyekiti wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa Jahazi iliotolewa na Jumuiya ya RAWWAZA kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akionesha Tunzo aliyokabidhiwa na Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar ( RAWWAZA) ya ‘Kumpongeza Mama Mariam Mwinyi Kwa Kuungana Nasi Zidi ya Kuwapigania Wanawake na Watoto Zanzibar’ baada ya kukabidhiwa na Walezi wa Jumuiya hiyo Mhe. Taufik Salim Turky na Mhe Faharia Khamis Shomar. Wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii Ili Kutengeneza Kesho Yako.(Picha na Ikulu)
KIJANA Suleiman Said Humoud akitowa ushuhuda yaliomkuta wakati akitumia dawa za kulevya na athari alizozipata wakati wa matumizi hayo na kupata msaada kupitia Jumuiya ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar( RAWWAZA) na sasa ameachana na matumizi ya Dawa za Kulevya, akitowa maelezo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza mmoja wa shuhuda wa matumizi ya Dawa za Kulevya Ndg. Suleiman Said Humoud akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wa Mradii wa Jumuiya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar wa Amka Mwanangu Soma kwa Bidii, uliozinduliwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Malindi Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwake) Mwenyekiti wa Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tauhida Cassian Gallos.(Picha na Ikulu)
No comments: