KUSHEHEREKEA SIKU YA MADJ DUNIANI NCHINI 2020
Chama cha muziki wa Disco Tanzania (TDMA) Kwa kushirikiana na Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF) Wanapenda kuwafahamisheni kuwa Mh Dr Hassan Abass Katibu Mkuu wizara ya habari, utamaduni Sanaa na michezo ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya Jumapili ya tarehe 14/03/2021 kwenye kusheherekea siku ya MADJ Duniani ambayo itakuwa ni kwa mwaka wa tano kusheherekewa hapa nchini. na kwa mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika kwenye ukumbi namba moja kwa burudani hapa nchini waMaisha Basemet (THE BASSE) Uliopo kwenye jengo la Millenium Tower lililopo maeneo ya Makumbusho Dar es salaam kuanzia saa 5 usiku mpaka majogoo.
TDMA Kwa kushirikiana na Shirikisho la Muziki Tanzania TMF Wamekusudia kutoa tuzo kwa Ma Djs mahiri wa zamani na wa sasa ambao wametoa mchango mkubwa katika tasnia ya Udj hapa nchini Pia TDMA na TMF wamekusudia kuwasaidia Dj wa sasa kuwa na mwamko mzuri katika maisha na kutumia fursa mabalimbali katika kujiendeleza. sherehe hizo pia zitaambatana na kutambua michango mbalimbali na mafanikio ya MaDJs kati ka kukuza tasnia hiyo muhimu.
Sherehe hizo ambazo zimelenga kuwafikia wadau mbalimabali wa tasnia hiiyo na hasa kuhamasisha kizazi cha sasa kuwa na maadili mema ya Taifa na kulinda heshima ya sanaa hiyo. Maadhimisho hayo yataambatana na burudani na shuhuda mbalimbali kutoka kwa Madj waliofanikiwa na kudumu kwa muda mrefu kwenye tasnia hiyo huku wakipambana na changamoto mbalimbali. Pia TDMA Inaiomba Serikali kutengeneza mfumo wa kila Dj hapa nchini kuwa na leseni za kufanya kazi zitakazotofautiana kitaaluma kutokana na umahiri wa kila Dj.
Maadhimisho ya mwaka huu yameandaliwa lengo likiwa ni kuwakutanisha Madj wote kuungana kwa pamoja na kuweza kuwahamasisha wanajamii kujiunga na bima ya afya pia kupanda miti na maua ili kuweka mazingira katika hali ya usafi na kupendeza, kuihamasisha jamii hususani vijana kuepukana na kujiepusha na makundi mbalimbali ambayo ni hatarishi ni hatari katika jamii ya watanzania,pia TDMA Kwa kushirikiana Shirikisho la Muziki Tanzania, wanawahasa wazazi na walezi pamoja na jamii kwa jumla kuwa na jamii yenye maadili mema hususani vijana wenye stadi za maisha na kuishi maisha ya upendo na ya kiroho.
Pia TDMA kwa kushirikiana na TMF Inawahimiza waajili na Madjs wote hapa nchini kuzingatia kuingia mikataba ya kazi, kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na Bima ya afya, ili kuwawezesha kufanya kazi zao kisheria na kuepukana na waajili ambao wametokea mara kwa mara kutotoa haki stahiki kwa Madjs hapa nchini kwani waajili kutofanya hivyo ni kutowatendea haki ya msingi kisheria Madjs ambao ni kundi mojawapo la jamii ya ki Tanzania na fani yao ya Udj wanayofanya ni sehemu ya ajira ya kujipatia vipato vyao halali vinavyowawezesha kukidhi adhima ya Taifa ya kujitegemea.
Maadhimisho ya sherehe hizo yatawajumuisha madj mbalimbali kutoka katika vituo vyote vya Radio, Nightclub, Lounge, Bar, Discotheque, roadshow, Simba Scratch DJ academy, Pro 24 Dj Academy, Itch DJ Academy na sehemu mbalimbali pia maadhimisho hayo yatasindikizwa na burudani za kustukiza toka kwa wasanii wa Bongofleva na vikundi mbalimbali vya Kucheza muziki wa Disco dancers katika mitindo ya BBoy, Blackdance, Harlem shake shekisheki, Afro pop, Dag na ngoma za asili toka One family ARTS Group, Tiger group na BDS Crew na pia Madansa wengineo ambao waliwahi kushinda mashindano ya Taifa kama vile Athumani Digadiga, Kelly John, Sheba doo, Michael Jackson wa Tanzania, Sister Ney, Black Kwasakwasa na makundi mengineyo wataungana na madj katika maadhimisho hayo ambayo yataanza saa saa 5 usiku burudani itaendelea mpaka majogoo pia Madjs wataonyesha utundu wao Dj Skills kuchezea mashine kwa mixing za nguvu na scratching huku wakiwachezesha wapenzi waliohudhuria kwenye Dancing floor. Baadhi ya Madjs watakaoonyesha mautundu yao ni pamoja na Dj Mario, Dj Cobo, Dj Hunter, Dj Poddy, Dj Nature, Dj Besta, Dj Roger Kiss, Dj Easy Untorchable, , Dj Ommy Crush, Dj Danny, Dj Drumer, Dj Brayo, Dj Baddlytz, Dj Rama G, Dj Max, Dj White wakishua, Dj Besta, Dj Masauti, Dj Paschal Kitigwa, Dj Nature, Dj Perez Dj Crush selecta Dj Musa na MaDj wa kike Mona na DJ Dee Y ambao ni Ma dj wa kike TDMA Inaendelea kupokea majina ya madj mbalimbali washiriki katika tamasha hilo.
Ahsante
Tunatanguliza shukrani zetu
Asanterabbi Mtaki
Katibu Mkuu TDMA Taifa
No comments: