DK NDUMBARO : TUNAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI ZAIDI KATIKA SEKTA YA HOTELI ZA KULALA WATALII .
Na John Nditi, Morogoro
SERIKALI inawakaribisha wawekezaji zaidi katika ujenzi wa hoteli za kitalii na kutakazilizopo kuboresha huduma zake kwa gharama nafuu ili kila Mtanzania aweze kutalii katika hifadhi mbalimbali za Taifa nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro alitoa kauli hiyo wakati akifunga na mkutano wa siku nne uliomalizika mjini Morogoro wa wadau wa Utalii kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini.
Wadau waliioshiriki kwenye mkutano huo wa siku nne ni pamoja na wa Uwindaji wa Kitalii, Wasafirishaji Watalii, Waongozaji Watalii na Wakala wa Safari za Ndege , Watoa huduma za Malazi, Wadau wa Usafirishaji wa Anga na Meli.
Katika hitumisho ya mkutano huo Dk Ndumbaro ,alisema bado kuna hoteli za kutosha katika hifadhi zetu mbalimbali nchini na kwamba Serikali inaendelea kukaribisha uwekezaji zaidi katika sekta ya hoteli kwa ajili ya kutoshereza malazi ya idadi yoyote ya watalii .
“ Ukitembelea mbuga za Taifa unaweza kulala hoteli ya dola 9,000 kwa siku moja na pia unaweza kulala hoteli kwa Sh 30,000 huo ni uwezo wa mtu mwenyewe tu ul;ale wapi , kwa hiyo hoteli zipo nyingi za viwango tofauti ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata stahiki yake na ahdi kwenye Tent Camps watu wanalala” alisema Dk Ndumbaro.
Waziri Dk Ndumbaro, alisema; “ Na ndiyo maana Machi 5 , 2021 tulikuwa hapa nawadau wote wa mahoteli na tumeongea mambo mengi ikiwa na kuboresha hudunma zao kwa gharama nafuu ili kila Mtanzania aweze kutalii” alisema Dk Ndumbaro.
Dk Ndumbaro alirejea hotuba ya Rais Dk John Magufuli katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 12 la Novemba 13, 2020 alisisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya utalii nchini ili iweze kuchangia zaidi katika pato la Taifa.
Kwa mujibu wa Waziri wa Malisili na Utalii , katika hotuba hiyo, Rais alitoa dira ya kufikia lengo la watalii millioni tano sambamba na kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii kufikia Dola za Marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.
Waziri Dk Ndumbaro , alisema masuala ambayo pia, yamesisitizwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, hususan katika ibara ya 67.
Hivyo alisema kuwa Utalii ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ambayo inachangia zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yote ya nje na asilimia 60 ya mapato yote yatokanayo na biashara za huduma.
Kwa upande wake Mdau wa Utalii wa muda mrefu na mwanzilishi wa huduma za ya utalii wa Puto ( Balloon Safaris) kupitia Serengeti Balloon Safari , Jimmy Mkwawa , alisema katika mkutano na waziri wadau wa utalii wamewasilisha kwa maandishi na uchanagiaji kuhusu changamoto kubwa ya utitiri wa kodi na pia mawasilisho yaliyofanyika kwenye vikao mbalimbali kwa nyakati tofauti kushindwa kufabnyiwa kazi na kuwa ni kikwazo cha uwezakano wa kuongezeka kwa idadi ya wataalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro ( kati kati ) akijadiliana jambo na Mdau wa Utalii wa muda mrefu na mwanzilishi wa huduma za ya utalii wa Puto ( Balloon Safaris) kupitia Serengeti Balloon Safari , Jimmy Mkwawa , ( kulia) mara baada ya Waziri huyo kufunga mkutano wa siku nne wa wadau wa Utalii kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini iliofanyika mjini Morogoro.
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) , Mabula Misungwi Nyanda , ( kulia mtari wa mbele) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro ( hayupo pichani) ya ufungaji mkutano wa siku nne wa wadau wa Utalii kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini iliofanyika mjini Morogoro.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Uhifadhi wa TANAPA wakitoka uumbini mara baada Waziri wa Malisaili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro ( hayupo pichani) kufunga mkutano wa siku nne wa wadau wa Utalii kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii nchini iliofanyika mjini Morogoro.( Picha na John Nditi).
No comments: