ZOEZI LA UPANDAJI MITI YA KOROSHO ULYAMPITI LASITISHWA


MKUU wa wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Edward Mpogoro amesitisha zoezi la upandaji wa miti ya zao la korosho kwenye eneo alilokabidhiwa mwekezaji na serikali ya Kijiji cha Ulyampiti hadi hapo mgogoro wa maeneo ya mipaka kati ya vijiji vya Mwau na Ulyampiti utakapotatuliwa.

Mpogoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Ikungi alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo lililotengwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha zao la korosho.

Aidha mkuu huyo wa wilaya hata hivyo alisisitiza pia kwamba kutokana na mgogoro uliopo katika eneo hilo ni marufuku kwa viongozi wa serikali za vijiji hivyo kuendelea kukata na kugawa maeneo kwa wananchi au wawekezaji wenye ni ya kulima zao hilo la kibiashara.

“Sasa ndugu zangu pambaneni mlime, wewe ambaye hujapalilia nenda ukapalilie usije ukauwa watoto, ila pia kwenda kujikatia maeneo sasa mengine wenyewe ni marufuku kwa sababu kuna mgogoero kwenye maeneo haya kati ya mipaka asije akatoka mtu huko akaenda kufyeka,………………………..''

Yule ndugu yangu aliyesema amepewa ekari 80,usiendelee kwanza na ile biashara ya ekari 80 na pale ulipofyeka hewala, ambako hujafyeka usiendelee kufyeka kwa sababu maeneo haya yana mgogoro.”alisisitiza mkuu wa wilaya huyo.

Hata hivyo Mpogoro alitumia fursa hiyo pia kuuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na kamati za watu watano watano kutoka katika vijiji vya Mwau na Ulyampiti kuunda kamati ya kushughulikia mgogoro wa mpaka wa vijiji hivyo na kwamba wakati zoezi hilo likiendelea wananchi kwa upande wao wataendelea na shughuli za kilimo kwenye maeneo yao waliyokuwa wakiyatumia.

“Sasa katika kipindi hiki natoa maagizo kwanza kwa mtaalamu kwa maana ya Halmashauri na vijiji vyote viwili mtatengeneza kamati zote mbili zote mbili,wajumbe watano watano kila kijiji kushughulikia mpaka ila wananchi mkumbuke mtu mwenye maisha mi mpaka siyo wa kwake,tukishajua suala la mpaka ndiyo tunakuja   kuangalia docments alizonazo”alifafanua Mpogoro.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye eneo lenye mgogoro wa mipaka,baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mwau,walisema kwamba mgogoro huo wa mpaka umetokana na uongozi wa kijiji cha Matyuku kugawa eneo kwa mwekezaji bila kuushirikisha uongozi wa Kijiji cha Mwau.

“Kwa sababu migongano ya mipaka siyo hapa tu bali wengi tu wanagongana kwa suala la mipaka sababu ya kutoshirikishana, sasa mimi ningekuomba mheshimiwa DC kwa kuwa leo unakanyaga ardhi hii tupe uamuzi kama si watu wa Ulyampiti utuambie kama ni wa Mwau we angalia mwenyewe mpaka Ulyampiti uko wapi na Mwau uko wapi?alihoji kwa msisitizo Shabani Irunde Kijanga. 

No comments: