UJUMBE MZITO WA RAIS MAGUFULI KWA WATANZANIA WAKATI AKIAGA MWILI WA MHANDISI JOHN KIJAZI JIJINI DAR ...
*Atangaza siku tatu za kumuomba Mungu kuanzia leo
*Asema kwa Mungu hakuna kinachoshindikana kwake , awatoa hofu
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS Dk.John Magufuli amewataka Watanzania kuondoa hofu katika kipndi hiki kigumu huku akitangaza siku tatu kuanzia leo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu ii atuvushe na kuyashinda majaribu ambayo nchi inapitia kwa sasa.
Amesema kwa Mwenyezi Mungu hakuna ambacho kwake kinashindikana kwani mwaka jana baada ya kuibuka janga la Corona ,Watanzania walifanya maombi na wakishinda na hata mwaka huu bado anaamini maombi ndio yatatuvusha na kushinda tena.
Rais Magufuli ametoa ujumbe huo leo Februari 19,2021 katika Viwanja vya Karimjee wakati akitoa salamu fupi kwenye shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Dk.John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17 mwaka huu.
Amesema hivi "Niwaombe Watanzania matatizo yanapotoke tuwe wamoja, tushikamane.Hofu ni mbaya mwaka jana 2020 ugonjwa huu wa kubanwa kifua tuliushinda kwasababu ya kumtanguliza Mungu kwa kufanya maombi, tumefika mahali sasa tunatishana sana.
"Leo nimetumiwa ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi na Waziri wa Fedha Dk.Mpango ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Dodoma akiendelea na matibabu, naomba meseji yake niisome.
"Mheshimiwa Rais , nimepata jumbe wako kupitia mke wangu, hao wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu kwenye maombi yangu jana jioni.Naungana nawe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu Mhandisi John Kijazi...huo ndio ujumbe wa Waziri Mpango ambaye anazushiwa amekufa, lakini jana amewaombea msamaha kwa Yesu wanaomzushia.
"Magonjwa yapo na yataendelea kuwepo, na haya kuanzia hapa, kuna nchi zimepoteza watu wake wengi.Hivyo tuchukue tahadhari na kumtanguliza Mungu, tumefika mahali hata watu wanasita kutegemea nguvu za Mungu na wanategemea nguvu za binadamu, Mungu yupo."Rais Magufuli amesema watanzania tuedelee kusimama na Mungu kwani walishinda mwaka jana(2020)."Na huenda hili ni jaribu lingine , tukisimama na Mungu tutavuka, inawezekana kuna mahali tumemkosea Mungu, tusimame na Mungu.
kufa tutakufa tu, kwani kufa kupo, unaweza kufa na Malaria, Kansa au na magojwa mengine lakini kamwe tusimuache Mungu."Ndugu zetu Waislamu walitangaza muda wao wa kuomba, niliambiwa na Muft , Watanzania tuanze kwa leo kwa ndugu zetu Waislamu.Tumuombe Mungu kwa siku tatu, kuanzia leo Ijumaa , kesho Jumamosi na kumalizia Jumapili, naamini tutashinda.
"Tuhanagika sana, Mungu ni mwenye uwezo wa kila kitu, viongozi wa dini endeleeni kuhimiza maombi, tulishinda mwaka jana, tutashinda mwaka huu na tutaendelea kushinda miaka yote, mwaka jana tumeingia kwenye majaribu na tuliingia uchumi wa kati, miradi iliendelea, hata sasa hakutakuwa na Lock down.".
No comments: