RC NDIKILIO AMALIZA UTATA MGOGORO WA WAFANYABIASHARA WADOGO SOKO LA PICHA YA NDEGE KIBAHA

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa kushoto akiwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege kulia Mussa Ndomba wakati katika eneo la zamani la soko la picha ya ndege wakiligagua wakati wa zira yake ya kikazi kwa ajili kwenda kujionea eneoa la zamani pamoja na eneo jipya lililotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndkilo akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara mbali mbali wa eneo la picha ya ndege hawapo pichani kuhusiana na tamko la serikali juu ya kuhamamia katika soko jipya ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza wakati ujenzi wa upanuzi katika barabra ya morogoro ukiendelea.

Diwani wa kata ya Picha ya Ndege ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha Munssa Ndomba akifafanua jambo kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao walihudhulia katika mkutano wa kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha Jenipher Omolo akitoa ufafanuzi kwa wafanyabiashara wa picha ya ndege kuhusina na jinsi gani miundombinu ya soko hili itakavyoboresha pamoja na mikakati mbali mbali ambayo wamejiwekea katika kuwasaidia wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhandisi Martini Ntemo akizungumza na wananachi pamoja na wafanyabiashara mbali mbali wa picha ya ndege kuhusiana na soko hilo jipya ambalo limetengwa kwa ajili ya kuwasaidia kuendesha shuguli zao, Mmoja wa wakinamama ambao pia ni wafanyabiashara ndogondogo akizungumza jambo na waandishi wa habari sokoni hapo kuhusina na mwenendo mzima wa changamoto mbali mbali amabazo zinawakabli,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

*********************************************

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi  Evaristi Ndikilo hatimaye amemaliza sakata la mgogoro wa siku nyingi lililokuwa linawakabili wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Picha ya ndege Wilayani Kibaha baada ya kuingilia kati na kutoa tamko  na msimamo  wa  serikali la kuwaondoa   watu  wote  ambao  bado walikuwa  wamegoma  kuondoka katika eneo  la mradi wa upanuzi wa barabara kuu ya morogoro.

Ndikilo ametoa kauli hiyo  bada ya kuwep kwa hali ya sintofahamu na kuamua kwenda kusuluhisha jambo hilo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ambao amewataka wafanyabisha wote wa picha ya ndege kuhama mara moja na kwenda katika eneo maalumu ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya kuendeshe shughuli mbali mbali za biashara

Aidha Mkuu huyo aliongeza kuwa eneo hilo ambalo hapo awali walikuwa wafanyabiashara  wanafanyia shughuli zao lipo katika eneo la hifadhi ya barabara ya morogoro hivyo ni hatarishi sana kwa usalama wa maisha yao ukizingatia na magari mbali mbali yanapita karibu na eneo hilo.

“Kitu kikubwa ambacho leo nimekuja na kamati yangu ya ulinzi na usalama ni kwa ajili ya kuweza kujionea hali halisi pamoja na kujiridhishwa maana kumekuewepo na mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakisemwa na wafanyabishara hawa lakini nilishatuma timu yangu na imeniletea majibu kwa hivyo kitu kikubwa ni kuwaeleza kuwa eneo hilo lipo katika hifadhi ya barabara na ni hatarishi sana kwa maisha yetu.

Ndikilo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inawawekea mazingira rafiri ya kufanyia kazi wajasiriamali wote bila ya kuwabagua na sio kwa nia ya kuwaonea na kwamba eneo jipya ambalo limetengwa kwa ajili ya soko litakuwa la kudumu lengo wafanyabishara waweze kufanya kazi zao bila kusumbuliwa.

Kadhalika ndikilo aliwaonya baadhi ya wafanyabiashara ambao bado wanafanya shughuli zao katika maeneo ya vichochoroni ambayo sio rasmi na kuwataka wote kuhakikisha wanahamia katika soko hilo jipya ambalo litakuwa na miunndombinu rafiki ambayo itaweza kuwafanya kuendesha shughuli zao mbali mbali bila matatizo yoyote.

Pia aliziagiza mamlaka mbali mbali zinazohusika ikiwemo Dawasa, Tanesco pamoja na Tanrods kuhakikisha kwamba wanapeleka huduma katika eneo hilo la soko ikiwemo suala la upatikanaji wa maji safi na salama, suala la kuwepo kwa nishati ya umeme kwa bei ambayo ni rafiki kutokana na eneo hilo la ni muhimu kwa wafanyabiashara.

Kwa Upande wake Diwani wa kata ya picha ya ndege ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kibaha ameiomba serikali kuhakikisha inawaboreshea huduma ya miundombinu ya barabara na choo,na  uwepo wa stendi, maji pamoja na umeme ili wafanyabiashara hao waweze kuendesha shughuli zao katika mazingira ambayo ni rafiki.

 

Nao baadhi ya wafanyabishara  ambao wamekubali kuhamia katika soko  jipya la picha ya ndege licha ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani lakini hawakusita kuzungumzia changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika kujipatia kipato zikiwemo za mambo ya huduma ya choo pamoja na baadhi yao kuuzia bidhaa zao katika maeneo ya vichochoroni.

 

WAFANYABISHARA  wadogowado waliokuwa wanafanya shughuliza zao katika soka la Picha ya  ndege Wilayani Kibaha mkoani Pwani hapo awali waligoma kuondoka katika eneo hilo ambapo kwa sasa baadhi ya wameweza kutii amri ya serikali na kuweza kuhamia katika eneo maalumu ambalo tayari limetengwa.  

No comments: