RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA SALA YA IJUMAA MSIKITI WA MIEMBENI.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu) WAUMINI wa Kiislam wakifuatilia Khutuba ya Ijumaa ikitolewa na Khatibu Sheikh Khalid Ali Mfaume Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar (hayupo pichani) iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja (Picha na Ikulu) /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia Khutuba ya Ijumaa ikitolewa Khatib Sheikh Khalid Ali Mfaume ambae ni Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar (hayupo pichani) iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)
No comments: