MHE.KUNDO MATHEW AFANYA ZIARA NA KUKAGUA VITUO VYA UTOAJI HUDUMA YA MAWASILIANO KATIKA KITUO CHA SEACOM-TEGETA

 

Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Mh. Kundo Andrea Mathew akikagua miundombinu “man hole” ya usafirishaji huduma ya mawasiliano kwa njia ya bahari (wa pili kutoka kulia aliechuchumaa katikati)

Naibu Waziri,Wizara ya Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Mh. Kundo Andrea Mathew kifanya kikao na menejiment ya kampuni ya Zantel iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg.  Brian Karokola.

Naibu Waziri,Wizara ya Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Mh. Kundo Andrea Mathew akitoa maelekezo kwa muwakilishi wa kampuni ya SEACOM Mhandisi Silla Philip alipotembelea kituo cha utoaji wa huduma ya Mawasiliano kwa njia ya Mkongo Baharini (wa pili kutoka kulia)

*************************************

NA MWANDISHI WETU,

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Kundo Andrea Mathew afanya ziara na ukaguzi wa vituo viwili vinavyotoa mfumo wa Mawasiliano kutoka nchi kavu kwenda baharini kwa njia ya Mkongo akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania  TTCL Bw. Waziri W. Kindamba.

Mh. Naibu Waziri alianza ziara yake katika kituo cha SEACOM Jijini Dar Es Salaam leo, ambapo aliweza kupata ufahamu wa namna ambavyo Nchi ya Tanzania inavyosambaza mfumo wa Mawasiliano kutoka nchi kavu kwenda baharini kwa njia ya Mkongo. Mhandisi Silla Philip wa SEACOM alieleza pamoja na uwekezaji unaofanyika bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za ushindani hususani kutoka nchi jirani ambako wamewekeza zaidi katika mikongo ya bahari, muda mwingine zinatokea changamoto za miundombinu ya mfumo wa mkongo baharini kuharibiwa katika njia zipitazo meli.

Pamoja na changamoto hii Mhandisi alieleza pia changamoto ya vibali vya kuingia baadhi ya nchi kwa mafundi pale ambapo itahitajika mafundi kuingia katika baadhi ya maeneo hayo ya nchi. Mhe. Naibu Waziri aliyapokea yote na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo kwa kushirikiana na nchi jirani   ili pindi changamoto hizo zitakapotokea ziweze kutatuliwa mapema na kwa uharaka.

Baada ya kutembelea kituo cha SEACOM, Mh. Naibu Waziri aliweza pia kukagua kituo cha EASSY ambacho kinahifadhiwa na kampuni ya simu ya Zantel. Mhe. Naibu Waziri aliweza kufanya kikao kifupi na Menejimenti ambapo alipokea changamoto zilizoelezwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Ndg. Brian Karokola ambae alimkaribisha Mh. Naibu Waziri ambae alitoa pongezi kwa Serikali kutokana mandhari mazuri na shawishi inayovutia wawekezaji  nchini katika sekta ya Mawasiliano ukilinganisha na baadhi ya nchi zingine.

Mkurugenzi Mkuu alibainisha kwamba Tanzania ina utulivu katika siasa, uchumi unaokua pamoja na mfumo imara wa Mawasiliano nchi kavu na baharini na hivyo kufanya sehemu salama katika uwekezaji katika sekta ya Mawasiliano.

Hata hivyo Mhe. Naibu Waziri aliongezea kwa kusema changamoto ambazo zipo katika sekta ya Mawasiliano zinahitaji mazungumzo na uchambuzi wa kina baina ya wadau mbalimbali ili kuweza kuzitatua.

Aliwahakikishia kuwa changamoto hizi zote zitafanyiwa kazi na serikali ili kupitia sekta ya Mawasiliano kila mwekezaji apate faida.

“Hatutaki wawekezaji wateseke bali waweze kuwekeza  kwa Amani na faida, katika Sekta ya mawasiliano na Taifa linufaike na kodi za wawekezaji.” Mhe.Kundo.

No comments: