Makao makuu mapya ya halmashauri ya wilaya ya Njombe ni ruksa kujenga ghorofa

Na Amiri Kilagalila, Njombe
BARAZA la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe limeweka msimamo wa makao makuu ya halmashauri kujengwa kata ya Kidegembye na kuwatoa hofu wananchi juu ya uamuzi huo huku wakiwataka kuacha kupotoshwa na maneno ya baadhi ya watu mitandaoni wanaopindisha maamuzi hayo kwa malengo ya kuchafua taswira ya halmashauri.

Awali akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani katika ukumbi wa shule ya sekondari Mtwango yanakopatikana makao makuu ya muda ya halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Valentino Hongoli amesema anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wananchi wanaosambaza taarifa potofu juu ya ujenzi wa makao makuu yanayotarajiwa kujengwa kata ya Kidegembye huku wakidai makao makuu hayo yatajegwa kata ya Matebwe na wengine wakisema Lupembe wakati baraza la madiwani lilikwisha pitisha adhma yake katika kata ya kidegembye kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.

“Kuna habari zimeanza kulete mikanganyiko kwamba makao makuu ya halmashauri yetu sio Kidegembye,nimeshasema sisi ndio tulioaminiwa na wananchi kuja kuwawakilisha,wanaoamua kuyavuraga maamuzi ili kuleta mkanganyiko kwenye halmashauri yetu waache.” Alisema Hongoli

Aliongeza kuwa hatua ziliendelea mara baada ya uamuzi ikiwemo upimaji wa udongo na kupeleka taarifa zingine za ujenzi ikiwemo BOQ katika wizara ya TAMISEMI ambapo eneo hilo limekubalika kwa ujenzi wa majengo ya aina yeyote,na kuwataka wachache wanaopotosha kwa maslahi binafsi kuacha mara moja.

“Baada ya maamuzi ya makao makuu yetu kuwa kata ya Kidegembye,maandalizi mbali mbali yaliendelea na kazi ya upimaji wa udongo ilishafanyika,majibu yalitoka kwamba mahali pale tunastahili kujenga majengo ya aina yoyote hata gholofa inaruhusiwa.” Alisema Valentino Hongoli

Naye Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwirn Swale ametoa wito kwa madiwani kuendelea kuwa na misimamo ya pamoja na kuto kuyumbishwa na wachache mtaani kwa kuwa baraza ndilo lenye maamuzi.

“Jimbo letu sisi tumeambiwa tujenga makao makuu, tumeahidiwa fedha hatujapewa lakini niwaambie hiyo fedha itakuja wakati wowote kwa kuwa nimefanya kazi kwa hiyo uamuzi unaofanywa na sisi humu madiwani lazima tuusimamie.” Alisema Edwirn Swale.

Madiwani wa halmashauri hiyo akiwemo Oscar Kihombo diwani wa kata ya Mtwango amewaomba madiwani kuendelea kuwa wamoja kulingana na makubaliano ya baraza ili kuondoa mgawanyiko utakaoludisha maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameshauri baraza la madiwani kuendelea kuwa watulivu kutokana na maamuzi yao kwa kuwa wenye maamuzi ni wao badala yake waendelea kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya halmashauri.

“Watu watasema lakini kumbu kumbu zimeandika nini,ijengeni halmashauri halmashauri kwa kulinda yale mliyoyaamua na msifungue kufanya kazi na mitandao nawaomba tukae kimya na kama kuna maelekezo mengine yatakuja maelekezo rasmi”Alisema Ruth Msafiri

Halmashauri ya wilaya ya Njombe ni miongoni mwa halmashauri nchini zilizoelekezwa kusogea makao makuu na kufanya kazi karibu na wananchi na kuondoka maeneo ya nje ya utawala ambapo halmshauri hiyo awali ilikuwa ikipatika katika makao makuu yake katika eneo la halmsahauri ya mji wa Njombe ambapo tangu agizo la wiazara lilipotolewa kwa sasa makao makuu yake ya muda yanapatikana kata ya Mtwango inaposubiriwa kujengwa makao makuu mapya.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Valentino Hongoli akieleza msimamo wa baraza la madiwani juu ya ujenzi wa makao makuu ya halmashauri huku akieleza kusikitishwa na upotoshaji unaoendelea mitandaoni.
B:Viongozi wa meza kuu katika baraza la madiwani wakisikiliza baadhi ya hoja zilizokuwa zikichangiwa katika kikao cha baraza la madiwani.
C:Baadhi ya madiwani wakisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya wakati akizungumza juu ya maswala ya uboreshwaji wa elimu pamoja na kuhakikisha halmashauri hiyo inapambana na kufanikiwa kuwafikisha shuleni watoto wote waliofaulu kuanza masomo ya elimu ya kidato cha kwanza.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akifafanua na kuipongeza halmasahuri ya wilaya ya Njombe namna ilivyofanikiwa katika swala la ukusanyaji wa mapato pamoja na kuvutia wawekezaji.

No comments: