MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA BALOZI KIJAZI

 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi  katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la  aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  John Kijazi katika Mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya  Mtakatifu Augustino eneo la Manundu Korogwe, Februari  20, 2021. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimpa pole,  Francisca Kijazi,  Mjane wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi John Kijazi katika Ibada ya kumwombea marehemu  iliyofanyika  katika Kanisa Katoliki Parokia ya  Mtakatifu Augustino lililopo Manundu Korogwe, Februari  20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mawaziri wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye  Makaburi ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Augustino, eneo la Manundu  Korogwe, Februari 20, 2021. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  alimwakilisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika  mazishi hayo. Kutoka kushoto ni , Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Juma Aweso, Waziri wa Maji, Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesugulikia Muungano na Mazingira, Profesa  Joyce Ndalicako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia na kulia ni Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

No comments: