EQUITY BANK YAZINDUA NJIA MPYA ZA UTUMAJI NA UPOKEAJI WA PESA KIMATAIFA
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania Mr. Robert Kiboti akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika hafla fupi ya kutambulisha huduma mpya za kupokea pesa na kutuma kimataifa. Benki ya Equity imeungana na makampuni ya Kimataifa ya WorldRemit, Western Union, Terrapay na mengineyo katika kuhakikisha inapanua wigo wa huduma hizo duniani kote.
Tanzania inakisiwa kuwa na takriban wananchi milioni nne wanaoishi ughaibuni. Kwa mwaka, wananchi hao hutuma nyumbani Zaidi ya dola za milioni 437.
Akizungumza katika ghafla ya uzunduzi wa huduma hizo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti kuwa alisema huduma hizi zipo katika vipengele viwili; Kwanza ni huduma za upokeaji na utumaji Pesa nje yaani (Remittance services) ambapo Benki ya Equity inashirkiana na makampuni makubwa ya World Remmit, Western Union, Money Gram, Small World, SimbaPay, Transact, Terrapy and Thunes ili kuweza kutuma na kupokea pesa kwa nchi zaidi ya 250 duniani.
Huduma ya pili ni ya mfumo maalum wa ndani ujulikanao kama “inter country transfer” ambao unawezesha wateja wa Benki ya Equity kuweza kutuma fedha kwenda kwenye mtandao wa matawi yote ya Benki ya Equity katika nchi za Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Congo, na Sudani Kusini kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi elfu kumi kwa muamala usiozidi kiasi cha shilingi milioni Kumi.
“Tunafuraha kubwa kuzindua rasmi huduma hizi zenye lengo la kuwaunganisha watanzania waliopo nje ya nchi na familia zao hapa nyumbani. Tumejiwekea lengo la kutanua wigo wetu katika mtandao huu ili tuweze kuwafikia watanzania wote nje ya nchi kwa asilimia 100. Muunganiko wetu makumpuni haya makubwa katika tasnia yakutuma na kupokea pesa kama World Remits, Western Union yatatupa uwezo wa kufika kila kona ya dunia na kufikisha huduma zetu” alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Tanzania ni nchi ya tatu kwa Afrika Mashariki kwa mapato yatokanayo na watanzania waishio nje ikiwa nyuma ya nchi za Kenya na Uganda. Sehemu kubwa ya pato kutoka nje hutumika katika matumizi ya familia na uwekezaji katika miradi ya kiuchumi.
Kupitia huduma hizi, mteja au asiye mteja wa Benki ya Equity anaweza kuchukua fedha alizotimiwa kwa kuamua kuchukua taslimu au kuwekewa moja moja kwenye akaunti yake.
No comments: