DC CHONGOLO ATOA SIKU SABA SOKO JIPYA LA MAGOMENI KUANZA KUTUMIKA


 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akimsikiliza Mhandisi wa Manispaa anayesimamia ujenzi wa Soko la kisasa la Magomeni Elibariki wakati alipofanya ziara ya kukagua soko hilo mapema leo asubuhi.
Mwekahazina wa Manispaa ya Kinondoni, Maximilian Tabonwa akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo wakati wa ziara ya kukagua Soko jipya la Magomeni ambalo litaanza kutumika wiki ijayo.
Mwekahazina wa Manispaa ya Kinondoni, Maximilian Tabonwa akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, Mstahiki Meya Songoro Mnyonge wakati wa ziara ya kukagua Soko jipya la Magomeni ambalo litaanza kutumika wiki ijayo.

…………………………………………………….

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo ametoa siku saba kwa wafanyabiashara wa Soko la Magomeni kuanza kufanya biashara zao katika soko jipya la kisasa ambalo tayari limeshakamilika.

Mhe.Chongolo ametoa kauli hiyo leo (jana) wakati alipofaya ziara ya kutembelea soko hilo ambapo pamoja na mambo mengine ameridhishwa kukamilika kwa mradi huo na kwamba hivi sasa wafanyabiashara wote wanapaswa kuanza kulitumia.

Ameongeza kuwa mradi huo wa Soko lakisasa ambao umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 8.9 litakuwa chachu kwa wafanyabiashara wandani na wa Manispaa ambao walikuwa wakifanya shughuli zao katika soko la awali.

“Nimefurahishwa na kazi kubwa ambayo Manispaa mmeifanya,niwapongeze kwa kazi nzuri imeonekana, sasa wafanyabiashara wote niagize baada ya siku saba wote muwe mmesha anza kufanyashuguli zenu kwenye soko hili jipya, leo ni jumatano nimezungumza jumatano ijayo wote muwe hapa”amesema DC Chongolo.

Kwaupande wake Mwekahazina wa Manispa ya Kinondoni, ndug.  Maximilian Tabonwa amesema kuwa hadi sasa jengo hilo limekamilika kwa asiimia 99.9  na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni kuweka utaratibu kwa wafanyabiashara hao kuanza kuingia.

Ameongeza kuwa soko hilo linavizimba 320, maduka 150 ambapo yatahusisha wafanyabiashara wa matunda, nafaka, mbogamboga, karanga pamoja na wauza mitumba.

Mradi wa ujenzi wa soko la kisasa la Magomeni ni miongoni mwa miradi ya kimkakati katika Manispaa iliyopo chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.9 ikiwa ni gharama za usanifu ujenzi na usimamizi hadi uliopokamilika.

Hata hivyo mradi huo unaumuhimu ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira kwa wananchi, kuongeza vyanzo vya mapato katika Manispaa sambamba na kuboresha,kuweka mazingira mazuri na huduma ya miundombinu kwa wafanyabiashara wakubwa, wadogo na jamii kwa ujumla.

No comments: