BMU ZAPANDISHA MAPATO HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI
|
AFISA Uvuvi wa Mradi wa Swiofish wilaya ya Bagamoyo Yasinta Magesa akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Wajumbe wa BMU wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye soko la Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yao ya mafunzo
Jengo la BMU Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Issaya Mbeje amesema kuwa siri ya halmashauri hiyo kupaa kimapato katika makusanyo ya ushuru wa mazao ya bahari ni kutokana na kutumia vikundi shirikishi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi(BMU).
Vikundi Shirikishi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi(BMU) halmashauri ya wilaya ya Pangani vilianzishwa kupitia mradi wa MACEMP mwaka 2009 na utendaji wake unazingatia Sera ya Uvuvi ya sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Mwongozo wa kitaifa wa BMU wa mwaka 2005.
Mbenje amebainisha hayo katika ofisini kwake kwa ujumbe wa vikundi vya BMU kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Chandika Dismas Chandika pamoja na Mwenyekiti ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira katika ziara ya siku moja ambayo imedhaminiwa kupitia mradi wa SWIOFish Tanzania bara unaofadhiliwa na Benki ya Dunia(WB).
Mbali na Tanzania mradi wa SWIOFish pia unatekelezwa katika nchi za Msumbiji na Commoro.
Amesema kuwa wilayani humo maeneo manne ambao vikundi hivyo vinafanya kazi katika vijiji 12 katika ukanda ambavyo ni Mkwaja,Kipumbwi,Pangani Mashariki na Pangani Magharibi.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2014/15 BMU ilipoanzishwa walifanikiwa kukusanya fedha kiasi cha Sh.23.8 milioni,mwaka 2016 walikusanya Sh.35,517,290/-,mwaka 2016/17 walikusanya Sh.128,178.567/-na mwaka 2017/18 mapato yalipanda hadi kufikia Sh.256.8 milioni.
Alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19 baraza la madiwani katika halmashauri hiyo waliamua kuwapa kazi ya kukusanya mapato maafisa watendaji wa vijiji ambapo walifanikiwa kukusanya Sh.162.051,600/- na mwaka 2019/20 mapato yalishuka na kukusanya Sh.137,354,125/-.
“Katika miaka ya nyuma wakati tuanaanza kukusanya mapato ya mazao ya bahari tuliwatumia BMU mapato yalipanda sana lakini walipopewa watendaji wa vijiji mapato yalishuka,hivyo baadae baraza la madiwani likaona bora tuwatumie tena BMU ambao wanafanya kazi kupitia serikali za vijiji husika,hivyo tumezifufua na kuwajengea uwezo,kuwapa mafunzo ya kukusanya mapato kupitia shirika la SeaSense,”.
“Baada ya baraza la madiwani kufanya mapitio ya bajeti kuona mapato yanashuka,kamati ya fedha tulibainia mapungufu na kupitia upya mikataba ya BMU tukaona tuwape kazi ya kukusanya mapato ya mazao ya bahari ambapo katika kipindi cha kuanzia July 1 2020 hadi January 2021 tumeafanikiwa kukusanya Sh.93 milioni. Na BMU wakishakusanya mapato tunawapa kamisheni ya asilimia 10”.Alisema
Mwenyekiti wa BMU Pangani Magharibi John Frank Baya alisema kuwa safari ya kuanza kukusanya mapato ilianza mwaka 2014 kwa majaribio ya muda wa miezi 6 walifanya vizuri ndipo baraza la madiwani wakaona wawape kazi hiyo kabla ya baadae kuwapa watendaji wa vijiji kisha kuwarudisha tena.
Alifafanua kuwa siri kubwa ya mafanikio ya BMU katika kukusanya mapato ni kushirikisha wajumbe wote wa pamoja na kutoa elimu katika jamii ya kijiji katika kukusanya mapato ambapo wa natoa ushirikiano kutoka katika asilimia 10 wanayopata,asilimia 5 wanairudisha kijijini ambapo inasaidia kuduma za jamii.
“Tunapokusanya ushuru tunashirikisha jamii katika kijiji husika pamoja wajumbe wote wa BMU na kutoa elimu hivyo hawakwepi ushuru na wavuvi wenyewe tunawaelimisha faida ya ushuru ambapo pia unawasaidia wenyewe na wanatuelewa,”alisema.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo amsema kuwa kupitia BMU za Pangani wamefurahishwa na jinsi halmashauri hiyo ilivyoweza kufanikiwa kukusanya mapato ya mazao ya bahari kupitia BMU na kuahidi kuenda kutoa elimu kwa madiwani wa Bagamoyo na BMU katika kukusanya mapato katika rasilimali za bahari.
Kwa upande Adhri Mohamedi mvuvi katika eneo la Kipumbwi amebainisha faida wanazozipata kupitia BMU ni pamoja na kupewa msaada pindi wanapopata majanga.
“Tunapotoa mapato faida nyingine inarudi kwetu,kwa mfano hivi karibuni kuna mvuvi mwenzetu alipotea lakini tulitoa taarifa BMU walitusaida fedha na mafuta hadi tukafanikiwa kumpata,”alisema
No comments: