RAIS WA ZANZIBAR DK HUSSEIN ALI MWINYI AMESHIRIKI TAMASHA LA MAZOEZI YA VIUNGO ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Cheti cha Heshima Mshiriki namba moja wa Mazoezi Zanzibar, akikabidhiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) Ndg.Said Suleiman, wakati wa hafla ya mazoezi ya viungo ya pamoja yaliofanyika katikia Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar leo 1-1-2021.(Picha na Ikulu) WASHIRIKI wa Tamasha la Mazoezi ya Viungo Kitaifa Zanzibar Bi. Pili Mwalimu (kulia) na Bi.Kazija Othman wakimaliza matembezi ya Tamasha la Kitaifa la Mazoezi ya Viungo Zanzibar wakipita katikja jukwaa kuu la Viongozi katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar kumalizia matembezi hayo yalioazia katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani kisonge na kumalizia Uwanja wa Amaan kwa mazoezi ya pamoja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika Tamasha la Mazoezi ya Kitaifa ya Viungo Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkewe Mama Sharifa Omar Khalfan (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa wakishirika katika Tamasha la matembezi ya mazoezi ya Viungo Zanzibar, yalioazia katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Kisonge Jijini Zanzibar na kumalizia katika Uwanja wa Amaan.(Picha na Ikulu)
WASHIRIki wa Tamasha la Mazoezi ya Viungo la Kitaifa Zanzibar wakipita katika jukwaa kuu la Viongozi wakati wa kumalizia matembezi hayo katika viwanja vya Amaani na kujumuika katika mazoezi ya pamoja yaliofanyika katika uwanja huo leo 1-1-2021.(Picha na Ikulu)
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar wakishiriki katika Tamasha la Mazoezi ya Viungo la Kitaifa Zanzibar wakipita katika Jukwaa la Viongozi katika Uwanja wa Amaan, matembezi hayo ya mazoezi ya Viungo Zanzibar yamepokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) na kujumuika katika mazoezi ya pamoja yaliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WANAMICHEZO wa Kikundi cha mazoezi ya Viungo kutoka Mkoani Dodoma wakishiriki katika Tamasha la Mazoezi ya Viungo la Kitaifa Zanzibar wakipita katika jukwaa kuu la Viongozi wakati wa kumalizia matembezi hayo na kupokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) na kujumuika katika mazoezi ya pamoja yaliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, wakishiriki katika mazoezi ya pamoja ya viungo yakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Ndg. Omar Hassan King, baada ya kumaliza matembezi hayo katika viwanja vya Amaan Jijini Zanzibar, wakati wa Tamasha la Kitaifa la Mazoezi ya Viungo Zanzibar lililofanyika leo 1-1-2021.(Picha na Ikulu)MSHIRIKI wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar Bi. Halima Muhamad Othman (60) kutoka Kikundi cha Mazoezi cha Solution Fitness Club cha Magogoni Zanzibar akishiriki katika mazoezi hayo yaliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
No comments: