KOCHA SVEN ATUA MOROCCO KUINOA ASFAR RABAT
ALIYEKUWA kocha wa Simba SC, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na ASFAR Rabat ya Morocco.
Vandenbroeck amejiunga na timu hiyo Rabat siku moja mbili baada ya kuondoka Simba SC akitoka kuiwezesha kufuzu Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Jumatano ikiitoa FC Platinum kwa jumla ya mabao 4-1.
Katika kipindi cha mwaka mmoja na zaidi ya kuwa na Simba, Vandenbroeck ameiwezesha timu hiyo kushinda mataji matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC.)
No comments: