WORLD VEGETABLES CENTER WAZALISHA AINA 18 ZA MBEGU BORA ZA MAZAO TOFAUTI
MKURUGENZI wa World Vegetable Center Dr. Gabriel Rugalema amesema kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1997 hadi 2018 wameweza kuzalisha aina 18 za mbegu bora za mazao tofauti ( nyanya,ngogwe,mchicha,mnafu,
Aliyasema hayo jana na kueleza kuwa taasisi ya World Vegetable Center ya Arusha imefanikiwa kuwa na benki ya mbegu na kutunza aina 3000 ya mbegu za mboga mboga zinazoweza kutumika kwa miaka 20 ijayo zikiwa na ubora ambapo aliongeza kuwa taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1992 na kuwa imefanikiwa kutafiti na kutunza mbegu zaidi ya 3000 za mboga mboga zenye asili ya Afrika.
Dkt. Rugalema alisema kuwa Tanzania inazalisha asilimia tano tu ya mbegu za mazao ya mboga mboga zinazotakiwa kila mwaka hivyo kituo kimelenga kukuza uwezo wa nchi kutafiti na kuzalisha mbegu za mboga kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI.)
“Tumefanikiwa pia kuwafundisha wakulima na maafisa ugani wapatao 25,142 nchini Tanzania kupitia kituo chetu cha World Vegetable Center hapa Arusha “alisema Dkt. Rugalema.
Alisema Kituo kimefanikiwa kuzalisha na kuachia aina za mbegu kama nyanya (6), mchicha (5), kabeji isiyofunga majani (sukuma wiki 2,) mnafu (4) na ngogwe (1)
“ Taasisi yetu imejikita katika kuwasaidia wakulima wa Tanzania bara na Zanzibar kujifunza, kuanzisha na kuendeleza ulimaji wa mboga wa kibiashara,na tayari kwa upande wa Zanzibar tumefikia wakulima 7,500” alisema Dkt.Rugalema.
Aidha alisema Kituo cha World Vegetable Center kanda ya Arusha pamoja na kutoa mafunzo ya kilimo inatoa pia elimu na maonesho ya aina mbalimbali ili wakulima wajionee matumizi na faida za ubunifu na teknolojia bora za umwagiliaji wa matone (drip irrigation.)
Dkt.Rugalema alisema wanakabiliwa na tatizo la ufinyu wa ardhi ya kufanyia utafiti kwenye eneo hilo na kuomba Wizara ya Kilimo isaidie kituo kupata eneo jingine kwani eneo hilo limetumika kwa miaka 25 bila kupumzika.
“ Mbegu za nyanya tu zinakadiriwa kuchangia Dola za Kimarekani milioni 250 katika uchumi wa Tanzania kwa miaka mitano iliyopita pamoja na kuongeza ajira na pato la familia” alisema Dkt.Rugalema.
Aliongeza kusema jumla ya wataalam 400 kutoka nje ya nchi waliopata mafunzo kati ya mwaka 1998 na 2018 na wataalam zaidi ya 2000 kutoka ndani ya nchi wamepatiwa mafunzo kati ya mwaka 1994 hadi sasa.
World Vegetable Center kipo Tengeru Arusha kimefanikiwa pia kufundisha zaidi ya wakulima 200,000 Tanzania Bara na Visiwani elimu juu ya mazao ya mboga mboga ili kuinua uzalishaji wake na kuongeza kipato cha wakulima.
Alisema kuwa ,tutaweza kutumia fursa hii kuimarisha utafiti wa mazao ya mboga mboga na kuongeza ujuzi na weledi wa wataalam wetu ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vyetu vya kilimo ili sekta ya mboga mboga ichangie ipasavyo katika uongezaji tija na kuchangia pato la Taifa” ,pia tutaweza kutumia fursa hii kuimarisha utafiti wa mazao ya mboga mboga na kuongeza ujuzi na weledi wa wataalam wetu ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vyetu vya kilimo ili sekta ya mboga mboga ichangie ipasavyo katika uongezaji tija na kuchangia pato la Taifa.
No comments: