JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA KULA SAHANI MOJA NA MADEREVA WAZEMBE
*Afande Ndozero asisitiza abiria kupaza sauti pale wanapoona changamoto
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama wa Barabarani Kimesema kuwa hakitaki madereva wazembe wakati wakisafirisha abiria kwa kipindi chote.
Jeshi hilo licha ya kutaka madereva kuwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na upande wa abiria wanatakiwa kupaza sauti pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao kwa kupiga simu makao makuu ya Jeshi hilo Kikosi cha Usalama Barabarani.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu kwa abiria na madereva Mrakibu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Mossi Ndozero amesema kuwa madereva wanaokiuka sheria hawatavumiliwa kwa kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa kufuata sheria za usalama barabarani.
Mrakibu huyo amesema kuwa katika kipindi hiki madereva wamekuwa wakitumia njia ya kuongeza viti ambavyo ni madumu na mito katikati ya viti na viti.
Aidha amesema kuwa wananchi wahakikishe wanasafiri kwa nauli iliyopo kwa mujibu wa sheria kwa kuambizana kati ya abiria na abiria.
"Jeshi la Polisi tumejipanga pamoja na kufanya operesheni kwa kila siku kwa madereva wa mikoani pamoja na usafiri wa ndani ya miji kwa kuamini kuwa ajali za uzembe wa watu hazipatiwi nafasi"Amesema Afende Mosi
Jeshi hilo pia Kimesema kwa kipindi hiki cha sikukuu kwa madereva kuacha mazoea kwenda mwendo wa Kasi kwani kitengo cha taa kiko imara.
No comments: