TASAC YANG'ARA MSHINDI WA PILI TUZO ZA NBAA


Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja,  akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) Emmanuel Ndomba  tuzo ya mshindi wa Pili kwa upande wa taasisi za Serikali ya uandaji bora wa hesabu zinazoratibiwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) zilizofanyika jijini Dar es Salaam. uwasilishaji bora wa hesabu kwa mwaka 2019 kwa kutumia viwango vya kimataifa vya kutayarisha hesabu za Taasisi za Umma zilizotolewa na NBAA jijini Dar es Salaam.


*Mkurugenzi  Mkuu Ndomba ataka Tuzo ya Mshindi wa Kwanza 2021

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

SHIRIKA la Uwakala wa Meli(TASAC) limesema kuwa  ndani ya miaka miwili limeweza kupata ushindi wa pili uandaji  bora wa hesabu hali ambayo inafanya kuaminika na wananchi kuwa fedha zinatumika vizuri.

Hayo aliyasema Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Emmanuel Ndomba baada ya kuchukua tuzo ya nafasi ya pili ya uandaji wa Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu Nchini (NBAA) kwa mwaka 2019 zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Ndomba amesema siri ya kufanya vizuri  kunatokana na uandaji wa Hesabu kitaalam na wahasibu pamoja na kujua fedha za wananchi zinasimamiwa kwa umakini.

Amesema kwa ndani ya Taasisi za Serikali kupata ushindi wa nafasi ya pili sasa wanatafuta kuwa washindi wa kwanza katika Tuzo za mwaka 2021.

"Haya mafanikio yaliyopatikana ni ya watanzania wote kwa Shirika lao katika kuhakikisha fedha zinadhibitiwa na kuweza kuleta maendeleo kwa Taifa."amesema Ndomba.

Aidha amesema kuwa kupata Tuzo hiyo ni kutokana na kujiamini katika uandaji wa mahesabu na kutaka Taasisi zingine ziweze kuingia na kuona faida yake.

No comments: