SPIKA WA BUNGE AWATAKA WAHITIMU WA VYUO KUTOTEGEMEA AJIRA,BADALA YAKE WAANGALIE NAMNA MOJA YA KUWA WAAJIRI

 Na Pamela Mollel Michuzi, Arusha


Spika wa bunge la Jamhuri wa Tanzania Job Ndugai Mh. Job Ndugai amewataka wanavyuo kutotegemea Ajira na badala yake waangalie namna bora ya kuwa waajiri.

Mh. Spika ameyasema hayo Leo katika Mahafali ya 22 katika chuo cha uhasibu mkoani Arusha ( IAA)  wakati akiongea na wahitimu wa fani mbalimbali wapatao 1952 kutokana chuoni hapo.

Aidha Spika Ndugai amesema serikali ilitoa fedha kwa ajili ya  fani hizo kutolewa ikiwemo usimamizi wa fedha,usimamizi wa biashara  ,sayansi ya kompyuta ili waweze kutumia fursa hiyo kuajiri na siyo kutegemea ajira.

"Wasomi wengi wanachagua kazi chukueni mfano aliyejenga Hotel ya Ngurdoto ambapo mmefanyia hii hafla yenu ndg Yetu Mrema je angesubiri kuajiriwa Leo tungekuwa hapa' tunataka kuona wasomi mkibuni vitu kama hivi au zaidi kwa kuwa mmeshajengewa msingi katika Elimu yenu" Alisema.

Aliongeza kuwa katika watu wenye kuweza kubuni matumizi mazuri ya fedha ni wahasibu na wakitumia elimu walioipata wataisaidia jamii katika kubana matumizi na kuweza kuendana hali halisi ya maisha ya kitanzania.

Alitoa rai kwa chuo hicho kuharakisha ujenzi wa chuo katika jiji la Dodoma ili waweze watumishi wa umma wapate elimu hiyo muhimu  itakayosaidia  upanuzi wa elimu kwa kila mtumishi hususani  katika Usimamizi wa ,fedha pamoja na ujasiriamali.

Naye mkuu wa chuo hicho Prf Eliaman Sedoyeka alisema maagizo hayo yaliyotolewa na Spika wanayafanyia kazi ambapo alisema tayari wameshapata ekari zaidi ya tano jijini Dodoma ili kuhakikisha wanajenga Majengo ya chuo na kwa hatua waliofikia kwa sasa wanashughulikia vibali vya ardhi na mwakani wanaanza rasmi ujenzi.

Alisema haya ni mahafali ya 22 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na  kwa mwaka huu wamehitimu wanafunzi 1952 katika fani mbalimbali kuanzia ngazi ya astashahada, stashahada, shahada na shahada ya uzamivu.

Spika wa bunge la Tanzania,Job Ndugai watatu kulia akiwa ktk picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali,
Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai akikabidhi cheti cha pongezi kwa mhitimu aliyefanya vizuri katika mahafali ya 22 chuo Cha Uhasibu Arusha iliyofanyika katika hotel ya kitalii ya Ngurudoto,katikati ni Mkuu wa chuo hicho Prof Eliaman Sedoyeka
Wahitimu wa fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 22 chuo Cha Uhasibu Arusha yaliyofanyika katika hotel ya kitalii ya Ngurudoto

 

No comments: