KEEYWAY MOTOR WAINGIA MKATABA WA MWAKA MMOJA KUTHAMINI TIMU YA NYOTA FOOTBALL CLUB

 Na Woinde Shizza, ARUSHA 

KAMPUNI inajishughulisha na Utengenezaji wa pikipiki Keeway Motor imeingia Mkataba wakuthamini timu ya mpira wa miguu ya  nyota  football club iliopo  jijini  hapa.

Akiongea wakati wa kungia mkata na timu hiyo Msimamizi mkuu wa tawi la kampuni ya Keeway mkoani Arusha, Lydia Kaguru  alisema kuwa wameamia kutuamini timu ikiwa  ni njia moja wapo ya kuinua vipaji vya vijana.

Alisema wameingia Mkataba wa mwaka mmoja kudhamini timu hiyo na kila mwaka wanatarajia kutumia shilingi milioni 10 na Mkataba huo unaanza kufanya kazi January moja 2021, lakini kwakuwa wameshaingia Mkataba wameanza kuwapa vitu mbalimbali Kama jezi.

"Kampuni yetu aijaanza kuthamini michezo hapa bali  ,inasaidia timu mbalimbali Katika kila eneo ambalo tunatoa huduma ambapo sisi Kama sisi tunatengeneza pikipiki hizi pamoja na spea za pikipiki na tumezagaa katika nchi 85 duniani  ikiwemo hapa Tanzania." Alisema Kaguru

Alisema mbali na kudhamini pia wachezaji na mashabiki watapata nafasi za kujaribu na kutumia pikipiki zao bila malipo yoyote endapo watakuwa na uhitaji wowote wa usafiri. 

Kwa upande wake Meneja wa timu ya  Nyota  Thobias Julius alishukuru kwa uthamini huo na kubainisha kuwa timu hiyo awali ilikuwa ikipitiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukosa nauli za wachezaji za kwenda kwenye mechi,jezi pamoja na vitu mbalimbali.

Alisema kuwa msaada huo umekuja mda muhafaka kwani utawasaidia kupata nauli, jezi  hasa Katika kipindi hichi ambacho timu yao iliopo ligi ya mkoa kufanya vizuri Katika zilizobaki kumaliza mzunguko wa ligi.

Akizungumzia msaada huo  kaimu katibu Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha Emanuel Antoni  alisema kuwa wamepata faraja kuona kunawathamini wanajitokeza kudhamini timu za ligi za Chini pamoja na zile za mchamgani.

Aliwataka wasiishie  kuthamini timu hiyo bali wathamini na timu nyingine kubwa za mkoani Arusha ambazo zipo Katika nafasi za juu Kama  AFC iliopo ligi daraja la kwanza pamoja na zingine.

Naye nahodha wa timu hiyo aliwahaidi wathamini hao kufanya vizuri na kusema kuwa wanawahaidi hawaja waangusha.
Msimamizi wa tawi la kampuni ya pikipiki ya Keeway Motor, mkoa wa Arusha, Lydia Kaguru katikati akiongea na waandishi wa habari hii leo wakati wa kuingia makubaliano ya kudhamini timu ya Nyota football club  kulia ni kaimu katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha, Emanuel Antoni kushoto Meneja wa timu hiyo Thobias Julius.
Msimamizi wa kampuni ya Keeway Motor, Lydia Kaguru akimkabidhi jezi Meneja wa timu ya Nyota football club Thobias Julius Mara baada ya kuingia mkataba.

No comments: