SHIRIKA LA SOCIAL ACTION FUND (SATF) LAZINDUA MRADI MPYA WA 'TUWALINDE WATOTO' MKOANI RUVUMA





 

KUFUATIA idadi kubwa ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kushindwa kutimiza ndoto zao kwa kukatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugumu wa maisha na ukatitili uliokithiri katika jamii shirika la social action trust fund (SATF) limezindua mradi wa TUWALINDE WATOTO mkoani Ruvuma mradi ambao utatekelezwa katika halmashauri za wilaya ya Madaba, Nyasa na Songea vijijini .

Mradi huu unalenga kuwasaidia Watoto wanaoishi katika mazingira magumu unaofadhiliwa na mfuko wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unaolenga kuwasaidia Watoto wanaoishi katika mazingira magumu Pamoja na wazazi na welezi ili waweze kujitegenea kimaisha hapo baadae.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mradi  mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la SATF Bwana Nelson Rutabanzibwa   alisema kuwa mradi huo utatekelezwa katika Wilaya tatu ambapo utajikita kusaidia Watoto katika sekta za Afya, Elimu na Ulinzi wa Mtoto katika mazingira anayoishi hasa ambao wamekuwa yatima baada ya wazazi wao kufariki kutokana na ugonjwa wa ukimwi. 

Alisema kuwa SATF katika mkoa wa Ruvuma imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali lakini awamu hii inakuja na mradi huu ikiwa ni moja ya jitihada za kutaka kumkomboa mtoto anaye ishi katika mazingira magumu na kushindwa kutimiza ndoto zake.

‘’ kwa upande wa afya tutawasaidia Watoto walio katika mazingira magumu kupata Bima za Afya kwa kuwalipia katika mashirika ya Bima pamoja na kuwasaidia wasichana  waliofikia rika barehe kupata taulo za kike pamoja na kuwapa elimu wao na walimu ili waweze kuwa salama na kupata elimu sawa na vijana wa kiume.’’ alisema Rutabanzibwa. 

‘’Tunawasaidia pia Watoto hawa kuondoa vikwazo katika sekta ya elimu ambapo tunawapa mahitaji yote ya elimu ikiwemo vifaa kama madaftari tunawalipia ada  na michango mbalimbali pale inapobidi pamoja na kujenga uwezo katika kaya ili kuwasaidia kupata mahitaji yote mhimu ikiwemo chakula,'' alisema.

Kuhusu usalama wa mtoto ndugu Rutabanzibwa alisema watafanya kazi na madawati ya jinsia na kamati za watoto zilizo katika ngazi ya kata pamoja na waratibu wa ustawi wa jamii ngazi ya mikoa na halmashauri uhakikisha kuwa Watoto hawa wakati wote wanalindwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Uzinduzi wa mradi huu ulifanyika katika ukumbi wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasimi Bwana Emanueli Kasongo ambaye ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma aliwataka watendaji wa Serikali walioshiriki katika uzinduzi huo kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na shirika la SATF kuwasaidia Watoto kundokana na hali ya ugumu wa maisha. 

‘’SATF imeleta mradi ambao unalenga kuwasaidia walengwa ambao wamepoteza wazazi kutokana na ugonjwa wa ukimwi na niwaombe watendaji kuhakikisha tunaungana na hawa wenzetu katika kutekeleza mradi huu huku tukiendelea na afua za kuzuia maambukizi mapya hasa katika maeneo ya starehe ambako tunatakiwa kuendelea kutoa elimu na naahidi kutoa ushirikiano kwa SATF.’’Alisema Emanuel kasongo.

Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo walisema kuwa mradi huo unaweza kuwakomboa baadhi ya Watoto ambao wako hatarini  na wamekata tamaa ya kufikia ndoto zao kwa kukosa huduma mhimu kama elimu.

‘’Mradi wa tuwalinde Watoto uliozinduliwa leo ni mradi mhimu saana kwetu kwa sababu Watoto wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa haki za msingi kutokana na umasikini uliokithiri ambao kwa sehemu Fulani unachangiwa na vifo vya wazazi vinavyotokana na ugonjwa wa ukimwi.’’ alisema Victor Nyenza Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Ruvuma.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma Ndg. Shafii Kasimu  Mpenda  alisema kuwa uwepo wa msaada wa taulo za kike kwa mabinti waliofika umri barehe utawezesha Watoto hawa wanaoshi katika mazingira magumu kufanya vizuri katika masomo yao pindi wawapo shuleni. 

‘’Mradi utakuwa na msaada mkubwa saana kwetu karika wilaya ya Madaba kwa sababu sisi wilaya yetu ni lango la uchumi ambapo watu wengi wananingia na kutoka kwa kuwa tuna watoto wengi wanaokosa mahitaji ya msingi na tunaishukuru serikali kwa kuruhusu mashirika binafsi kuendelea kufanya kazi katika nchi yetu ili kuleta amaendeleo.’’alisema Shafii. 

 

Msimamizi wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma Mkaguzi  Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bi. Melinda Mgumba alisema kuwa mradi huo utasaidia kuondoa usiri mkubwa dhidi ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa Watoto kwa kuwa umejipambanua kutoa elimu kwa Watoto na wazazi dhidi ya umhimu wa kumlinda mtoto.

No comments: