MBUNGE WA MVOMERO AFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI YA TURIANI


Mbunge wa Mvomero Jonas Van Zeland akiwa katika wodi ya Wanawake kwa kuwajulia hali katika hospitali ya Turiani.
Mbunge wa Mvomero Jonas Van Zeland akiwa katika wodi ya wanaume wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Turiani.


Picha mbalimbali za Mbunge wa Mvomero Jonas Van Zeland akiwa katika ziara hospitalini hapo.


WANANCHI wanaopata huduma ya afya katika hospital ya Turiani  wilayani Mvomero wamesema huduma wanazopata katika hospitali hiyo ziko juu na kusababisha baadhi ya wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Wamesema kuwa wanashukuru ziara ya mbunge kufanya  katika hospitali hiyo huku wakisema gharama zilizopo zingepunguzwa kutokana na hali za maisha ya watu.

Wananchi wameyasema hayo wakati wa ziara ya mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeland.

Zeland baada ya kuwajulia hali Wagonjwa amesema  kuwa ataangalia namna  kuishauri serikali namna ya  kuwapunguzia gharama ili wapate matibabu tofauti na ilivyo sasa ikiwemo kuchelewa kupata huduma wawapo hospitalini.

Katika ziara hiyo ametembelea  katika  wodi za wagonjwa na kuzungumza nao ikiwa ni pamoja ya kuwatia faraja zaidi.

Zeland  amesema  atayafikisha changamoto hizo kwenye ngazi husika huku baadhi ya watumishi wakimueleza mbunge kuwa kwa kipindi cha miezi mitano hawajalipwa mishahara yao kutokana na hospitali kutegemea chanzo kimoja cha mapato ambacho ni fedha zinazotolewa na wagonjwa, hali ambayo imesababisha kukosekana kwa fedha za kulipa mishahara baada ya wagonjwa kupungua hospitalini hapo

No comments: