MAHAFALI YA MUHAS YAFANA, FANI 11 ZAONGEZWA KATIKA MASOMO

 

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Katika kuzingatia umuhimu wa kuongeza wataalamu wa afya katika fani mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko la ajira, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)  kimeongeza fani kumi na moja (11) katika ngazi ya uzamili.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof  Andrea Pembe wakati wa mahafali ya kumi na nne (14) tangu Chuo cha MUHAS kiwe Chuo Kikuu kamili mwaka 2007.

Prof Pembe amesema, fani hizo mpya zinatolewa kwa mara ya kwanza hapa nchini katika ngazi ya Uzamili na zitasaidia kuongeza na kujenga uwezo wa kutoa huduma muhimu hivyo kutoa ufumbuzi wa changamoyo mbalinbali na kuboresha sekta ya afya nchini.

Amesema, kwa mwaka 2020/21 kimeweza kudahili wanafunzi wa shahada ya kwanza mia nane ishirini na tano (825) na wanafunzi mia mbili sitini na nane (268) kwa ngazi ya Stashahada kwa programu za Afya ya Mazingira Radiografia ya Uchunguzi wa magonjwa, Teknolojia ya Viungo na Stashahada ya Juu ya Dematovenereolojia.

"Kwa mwaka huu udahili umeongezeka kwa asilimia 2.23 ukilinganisha na mwaka jana na udahili kwa programu za stashahada za Famasia, Sayansi za Ufundi Maabara ya Tiba na Uuguzi umefanyika kupitia Barazaa la Taifa la Elimu ya Ufundi ( NACTE)," amesema 

"Katika ngazi ya uzamili, mwaka wa masomo 2020/21 Chuo kimedahili wanafunzi 895 kwenye fani mbalimbali za uzamili ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 42," amesema

Aidha, Prof Pembe ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuendelea kutoa ufadhili kkwa wanafunzi wa uzamili ambapo katika mwaka wa masomo 2019/20 jumla ya wanafunzi wapya 160 walipewa ufadhili  ana nia matumaini ni kuona utekekezaji wa mpango huo utaendelea kwa miaka ijayo.

Ameishukuru serikali kwa kuwapatia kiasi cha Fedha Bilioni Moja (1,000,000,000) kwa ajili ya kulipia mizigo mbalimbali kiasi cha makontena 20 kwa ajili ya kituo Mahiri cha Magonjwa ya moyo na Mishipa ya Damy kwenye kampasi ya Mloganzila. 

Hata hivyo kufikia Oktoba 2020, jumla ya Bilioni 2.5 kilichoidhinishwa kama fedha za maendeleo kwa mwaka 2019/20 kama mchango wa serikali katika ujenzi wa kituo hicho hazijalipwa.

Amemalizia kwa kuwapongeza tena wote wanaohitimu leo na kuwatakia mafanikio mema katoka shughuli zao watakazoenda kuzifanya za kujenga taifa.

Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt Harrison Mwakyembe amesema katika kuimarisha mafanikio chuo kimeandaa mpango mkakati kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020-2025 katika maeneo makuu yatakayopewa kipaumbele.

Amesema, maeneo hayo ni katika kuongeza ubora wa mafunzo na ufundishaji, kuwaongezea uwezo watafiti ili waweze fanya tafiti bora na tija zaidi, kuboresha miundo mbinu na mapayo ya ndani, kuboresha rasilimali watu na usimamizi wake pamoja na kuimarisha na kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

Jumla ya wahitimu 1,146 wameweza kutunukiwa katika ngazi mbalimbali, kati ya hao 509 ni wanawake ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.3 na kufikia 44.4 na wanafunzi 251 wametunukiwa stashahada na Stashahada za juu katika fani mbalimbaku za afya na sayansi Shirikishi.

Pia, wahitimu 549, wamepata shahada ya kwanza na 333 shahada ya uzamili. Wahitimu 9 wametunukiwa shahada ya juu ya uzamili wa Sayansi maalumu na wahitimu wanne (4) wametunukiwa Shahada ya Uzamivu wa Falsafa ( Doctor of Philosophy).

Wanafunzi hao wote waliweza kutunukiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu Al Haj Dkt Ali Hassan Mwinyi.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa  ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Daniel Matata katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho. Mahafali ya Chuo cha MUHAS yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa  ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Lulu Sakafu katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho. Mahafali ya Chuo cha MUHAS yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

No comments: