WEMA SEPETU, LULU DIVA KUNOGESHA FAINALI YA MODEL MAONYESHO YA MERCEDEZ BENZ

 Na Khadija seif, Michuzi TV

 MBUNIFU wa Mavazi nchini, Ally Remtullah amesema hakuna janja janja kwenye kuchagua  model kwa ajili ya maonyesho yake.

Hayo yamesemwa wakati akizungumza na michuzi TV na kusema mara nyingi kumekuwepo na minong'ono kuwa wabunifu wamekua wakirudia model wenye majina jukwaani hasa wanapoandaa matamasha yao na huwa wana machaguo yao tayari.

"Model akiwa hatembei vizuri inasababisha hata nguo ya mbunifu kutoeleweka yani akitembea vibaya lazima nguo ionekane mbaya pia, kitu ambacho siwezi kukubaliana nacho Mara nyingi." Amesema Remtullah

 Remtullah amesema kwa Mara nyingine ameandaa tamasha lake ambalo amelipa jina la Mercedes benz ambalo litafanyika Desemba mwaka huu.

"Tamasha la Mercedes benz natarajia kulifanya Desemba mwaka huu, hata hivyo fainali ya kusaka model wakiume pamoja na wakike litafanyika Novemba 14 ukumbi wa Backet Masaki hivyo niwakaribishe vijana wenzangu kukimbilia fursa hiyo." Amesema Remtullah.

Ameongeza kuwa mchakato huo utakua na majaji wapatao watano kutoka fani mbalimbali ikiwemo wasanii pamoja na watangazaji.

"Safari hii madam Sema Sepetu,Lil oomy, Lulu diva, Mim Mars pamoja na Idris Sultan watasimamia vizuri kwa upande wa mchuano wa kusaka vijana ambao watalipamba jukwaa letu la Mercedes benz pale Serena hoteli jijini Dar es salaam Novemba 28."

Hata hivyo amesema akiwa Kama kijana anapenda kugawa fursa kwa vijana wenzake ili kusukuma gurudumu la maendeleo nje na ndani ya nchi kupitia sanaa ya ubunifu wa Mavazi.

"Nimekua nikitoa fursa kwa vijana nikiamini sisi vijana ndio." Amesema Remtullah.

No comments: