WATANZANIA WATEGEMEE MAGEUZI MAKUBWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

 

kulia Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akikagua gari iliyotoka site aina ya fuso lenye kufanya kazi ya kubeba kokoto,mchanga na mawe katika kazi za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, gari hilo lina uwezo wa kubeba tani kumi na tano, kushoto ni kaimu mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali.  
Aliyesimama Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya, akikagua mtambo aina ya Wheel loader wenye kazi ya kuchota kifusi, alipotembelea katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kukagua mitambo hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akitoa maelekezo ya kutumika kwa mtambo mpya unaotumika katika ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili isipate kutu wakati wa mvua.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiendelea na ukaguzi wa Mitambo inayotumika katika ujenzi na ukarabati wa Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji jijini Dodoma leo.

Katibu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesema, watanzania wategemee mageuzi makubwa katika kilimo cha umwagiliaji, kwani serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekata hiyo.

Bw. Kusaya ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa na ziara ya kikazi katika ofisi za Tume ya Taifa yaUmwagiliaji, ambapo amesema Serikali ina mpango wa kuboresha mundombinu yote chakavu katika sekta ya umwagiliaji na kufufua skimu za zamani na kuongeza skimu mpya.

Alisema pia ikiwemo kuongeza vyanzo vipya vya maji katika maana ya kujenga mabwawa na kutumia vyanzo asili vilivyopo kama mito, mabwawa  ya asili na maziwa hivyo mkulima atanufaika na kilimo cha umwagiliaji katika mazao ya biashara na chakula.

Sambamba na hilo, amesema Serikali pia imeona umuhimu wakuongeza wataalamu wa sekta hiyo katika ngazi za wilaya na itafikia ngaz iya kata na kijiji ili kuweza kumfikia mkulima kwani kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo cha uhakika na mkombozi kwa mkulima.

“wakulima watapata huduma za uhakika zaidi na kunufaika na kilimo cha umwagiliaji” Alilisita.

Awali, alipokuwa akizungumza na menejimenti yaTume ta ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Kusaya amewataka watumishiwa Tumeya Taifa ya umwagiliaji kufanya kazi kwa ushirikiano,na uhakika ili kuweza kufikia malengo ya mageuzi makubwa yenye tija katika sekta ya umwagiliaji.

Na baada ya hapo katibu Kusaya alikagua mitambo iliyopo katika ofisi za Tume hiyo inayotumika kujengea na kuboresha miuondombinu ya umwagiliaji.

No comments: