WATALII WA NDANI ZAIDI YA 80 WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

 

Watalii wa ndani kutoka benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja katika lango kuu la kuingia eneo la Hifadhi ya Ngorngoro.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Uhifadhi (Huduma za Utalii)  NCAA Bw. Paul Fisssoo akizungumza na waandishI wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ujio wa watumishi wa CRDB waliotembelea vivutio mbalimbali katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro tarehe 14/11/2020

Baadhi ya Watumishi wa Benki ya CRDB waliotembelea hifadhi ya Ngorongoro wakiwa katika eneo la View point eneo ambalo ni mahususi kuona kuangalia mamdhari nzuri ya   bonde la Ngorongoro.

 ………………………………………………………………………….

Na Kassim Nyaki-NCAA

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imepokea zaidi ya watalii wa ndani 80 kutoka benki ya CRDB kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani (domestic tourism).

Safari ya watalii hao  iliyoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imelenga kutoa hamasa kwa watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kutangaza vivutio hivyo ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza pato la Taifa.

Mkurugenzzi wa Masoko wa TTB Mindi Kasiga aliyeambatana na ujumbe huo amebainisha kuwa, ujio wa wageni hao ni muendelezo wa juhudi za Serikali kuhamasisha watanzania na wageni wa mataifa mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini ili kutoa hamasa kwa wananchi.

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee duniani, TTB kwa kushirikiana na NCAA tumeandaa programu hii ikiwa ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za Serikali kutangaza vivutio vyetu ndani na nje ya nchi na tunafurahi kuona kwamba muoamko wa Watanzania kutembelea vivutio vyetu umezidi kuimarika kila mwaka”), aliongeza Kasiga.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi mwandamizi wa UhIfadhi (huduma za Utalii) wa NCAA Bw. Paul Fissoo ameipongeza TTB na CRDB kwa kuleta kundi la wafanyakazi zaidi ya 80 kutembelea hifadhi hiyo kwa wakatii mmoja na kusisitiza kuwa utaratibu huo ni mfano mzuri wa kuigwa kwa mashirika mengine ya Serikali na Sekta binafsi kuandaa safari za pamoja na watumishi wao ili kutembelea vivutio vya hifadhi hiyo kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 11,800 pekee.

Eneo la Hifadhi ya ngorongro ni eneo lenye vivutio vya kipekee duniani ikiwemo Crater ya Ngorongoro yenye Wanyama wa aina mbalimbali zaidi ya 25000, utalii wa kiutamaduni, makumbusho yenye historia ya chimbuko ya binadamu wa kale zaidi duniani (Zamadam), nyayo za binadamu wa kale, pia ni eneo pekee ambapo unaweza kuwaona Wanyama wakubwa watano (Simba, faru, Chui, Tembo na Nyati)  kwa wakati mmoja katika eneo moja.

No comments: