Wanawake wahamasishwa kuchangamkia fursa kwenye kongamano
Mjasiliamali Bi. Leina Lemomo akizungumza kwenye 'Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. Kongamano hilo pamoja na mambo mengine lilijadili namna wajasiriamali wanawake walivyo kabiliana na changa moto za janga la corona kwenye biashara zao.
Mkurugenzi wa Bang! Magazine, Emelda Mwamanga akizungumza kwenye Kongamano la 'Woman of Influence, I'm Possible' jana kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. Kongamano hilo pamoja na mambo mengine lilijadili namna wajasiriamali wanawake walivyo kabiliana na changa moto za janga la corona kwenye biashara zao.
Na Mwandishi Wetu, Glou ya Jamii
WANAWAKE waamka na kuanza kujifunza kupitia wanawake wengine waliofanikiwa pamoja na watu wanaofanya vizuri kwenye biashara.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa The East Africa Bang House Media, Emelda Mwamanga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika kongamano la 'WOMAN OF INFRUENCE' lililoandaliwa kwa ajili ya wanawake kujifunza kwa wenzao waliofanikiwa katika biashara zao.
Emelda amesema kuwa kila mwaka wamekuwa wakiadhimisha shughuli za wanawake ili kuwajengea uwezo wanawake waachane na desturi ya kulia na changamoto kwenye biashara.
"Sasa tujifunze kwa wezetu ambao wamekazana wapo kwenye biashara, tupeane mawazo ili 2021 unapoanza tuone wanawake wana-'shine' katika biashara."Amesema Imelda.
Hata hivyo amesema wanawake wengi wamekuwa wakikata tamaa katika biashara kutokana na mawazo potofu katika biashara na kusema kuwa hawawezi lakini kupitia kongamano hilo wanawake watatoka na kitu cha kujivunia.
"Kongamano hili la wanawake tutatiana moyo ili tuweze kusimama na kujisimamia wenyewe katika biashara zetu bila kuwa na woga wowote.
Tunataka kubadili mtazamo au mawazo ya kuwa mimi siwezi, mi nitakuwa na hela siwezi, kwahiyo tumetaka tuibadilishe hiyo mitazamo hasi kwakuwa kila mtu anaweza na tunaposema hatuwezi ni kama tunamshushua Mungu kuwa umetuumba basi tuu lakini Mungu ametupa uwezo wa kufanya kitu na kikawa." Amesema Imelda.
Emelda amesema kuwa kila mwanamke anauwezo hata kama anapesa chache anaweza kufanya chochote na sio kukaa na kulalamika kila inapotokea changamoto.
Amesema kuwa kongamano la wanawake si la kupeana pesa bali ni la kupeana fursa na mahusiano mazuri na watu wengine ili siku moja mwanamke ashuhudie kuwa alipata mchongo kupitia mtu mwingine pamoja na kupeana fursa (Opportunity) kupitia mtu mwingine na kupata elimu kupitia mtu mwingine aliyefanikiwa.
Hata hivyo Emelda amewaasa wanawake kutokubweteka na wajisukume wasogee sehemu ili kama kuna mtu anakushika mkono usikike na sio kukaa tuu nyumbani bila shughuli yeyote ya kuongeza kipato.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa ZARA Tours, Zainabu Nansell akielezea changamoto katika biashara yake amesema kuwa kipindi cha ugonjwa wa Corona kwenye upande wa Utalii imekuwa ni changamoto sana lakini anaomba Mungu wakipata chanjo ya Ugonjwa huo shughuli za utalii zitakwenda vizuri.
"Pia tumeweza kukaa na kuangalia njia gani rahisi ya kuweza kufanya ili tuweze kuishi katika kipindi hiki kigumu, kwahiyo tumekuja na maandalizi kwaajili ya utalii wa ndani tunaisukuma na tumeweza kupata wateja wachache waweze kwenda kutalii." Amesema Zainabu
Hata hivyo amesema wanamkakati wa kuhamasisha watanzania zaidi waweze kwenye katika likizo ya Kristmasi waweze kwenda safari na kupanda Mlima Kilimanjaro.
"Tunajaribu kusukuma Watanzania kwa ajili ya utalii wa ndani na kuwaeleza kuwa tunambuga nzuri ambazo wanaweza kwenda na kujionea uzuri wa nchi yetu, tunawaomba watanzania njoeni twenzetu Serengeti na ZARA Tours."Amesema Zainabu
Kwa upande wa gharama Zainabu amesema kuwa ZARA Tours wanakifurushi ambacho ni gharama nafuu kabisa kwa watu sita ni laki nne na Nusu (450,000/#) ambayo unatalii ndani ya Tanzania kwa siku tatu na kwa siku 5 ni shilingi laki nane.
Hata hivyo Zainabu amefurahia hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupata tuzo ya ubora Afrika kwani imekidhi vigezo vyote vya kupata tuzo.
"Mimi nafurahia sana Serengeti inahadhi ya kuwa Hifadhi za taifa bora kwa Afrika inabidi sisi Watanzania tujivunie tunakitu kama hiki, twende tukaangalie Serengeti, Ngorongoro na hifadhi za taifa zote, Watanzania tunatakiwa kujivunia na tupende kwenda." Amesema Zainabu.
Licha ya hayo Zainabu ameiomba Serikali isaidie kutangaza vivutio vyetu vya taifa ili Watanzania waweze kuona tulichojaliwa katika hifadhi zetu za taifa.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Msafiri travel, leina Limomo amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye majadiliano na nchi zenye hifadhi za taifa ili waweze kuandaa bei kwaajili ya utalii wa Afrika (African Rates) ambazo zitamwezesha kila muafrika kutalii kwa bei moja endapo atatembelea hifadhi yeyote au kivutio chochote ndani ya bara la Afrika.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya ZARA Tours, Zainab Ansell akizungumza kwenye 'Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' jana kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. Kongamano hilo pamoja na mambo mengine lilijadili namna wajasiriamali wanawake walivyo kabiliana na changa moto za janga la corona kwenye biashara zao.
Mmoja ya manamke akichangia mada katika Kongamano la wanawake lililofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mjasiliamali toka sekta ya utalii, Bi. Leina Lemomo akizungumza katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria Kongamano la mwanamke mwenye ushawishi lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.
No comments: