ECOBANK TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUPIMIA UGONJWA WA KISUKARI

 

ECOBANK Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya kupima ugonjwa wa kisukari katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kutenga siku maalum kusaidia jamii.

Kwa mujibu wa Ecobank katika nchi zote 33 Barani Africa zenye benki hiyo zimekuwa zikitenga siku maalumu kula mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka.

Taarifa ya Ecobank kwa vyombo vya habari imeeleza mwaka huu wamejikita katika kusaia kuelimisha na kusaidia kupunguza janga la ugonjwa wa Kisukari kwa kushirikiana na NDC alliances kwa kuendesha kongamano na mjadala kuelimisha watu jinsi ya kula vizuri.

Pia kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara ilikuweza kujiepusha na janga hilo  la ugonjwa wa Kisukari. Kongamano liliendeshwa kwa njianya mtandao Kwa kuzingatia janga la Corona duniani.

"Kwa hapa Tanzania, Ecobank imeshiriki siku ya Sukari duniani kwa kupima wafanyakazi wao, Sukari, Blood pressure na uzito. Zoezi hili liliendeshwa na kampuni ya udalali wa huduma za bima (ARIS) 

"Ecobank Tanzania pia imetoa msaada wa vifaa vya kupimia ugonjwa wa Kisukari kwa hospitali ya Mwananyamala. Vifaa kama vile, Glucometers, BP machines na vifaa vya kupimia uzito (weighing machines) vilikabidhiwa kwa uongozi wa hospitali ya Mwananyamala,"amesema.

Akipokea vifaa hivyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Daniel Nkungu ameishukuru benk hiyo na kwamba vifaa hivyo vitaisdia  kwani vimetolewa wakati muafaka."Vifaa hivi  vitasaidia kutakua tatizo ka uhaba wa vifaa vya kupimia sukari hopitalini hapo."
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu(kushoto) akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Daniel Nkungu(kulia) kwenye hospitali ya Mwananyamala iliyopo kwatika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya siku ya Benki ya Ecobank.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu(kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa hosptali ya Mwananyamala pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Ecobank Tanzania wakati wa kutoa msaada wa vifaa tiba kwenye hospitali ya Mwananyamala iliyopo kwatika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya siku ya Benki ya Ecobank .
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Daniel Nkungu  akitoa neno la shukran kwa uongozi wa Ecobank Tanzania mara baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamala iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Benki ya Ecobank Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya mwananyamala mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali hiyo
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakishiriki siku ya Sukari duniani kwa kupima afya zao kama kupima Sukari, Blood pressure na uzito. Zoezi hili liliendeshwa na kampuni ya udalali wa huduma za bima (ARIS).

No comments: