WANAFUNZI VYUONI WAFAULU KWA KUSOMA KWA BIDII NA SIO KWA RUSHWA YA NGONO-NAIBU SPIKA
Na Grace Gurisha
NAIBU Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema wanafunzi wa vyuoni wafaulu kwa kusoma kwa bidii na sio kwa rushwa ya ngono, kwa sababu ndiyo viongozi wa badae wanatakiwa wawe na uwezo mkubwa wa kuongoza wengine.
Dkt. Tulia esema hayo Leo Novemba 25,2020 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliyoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF).
Amesema hali ya kwenye vyuo sio nzuri sana katika masula ya ukatili wa kijinsia, katika Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeeleza kuwa katika vyouo ambavyo ilitembea na kuwahoji zaidi ya asilimia 50 wamepitia kwenye ukatili wa kingono.
Naibu huyo, amesema asilimia hiyo ni kubwa sana kinachotakiwa ni wanachuo kusoma na sio kufaulu kwa sababu ya rushwa ya ngono, mwisho wa siku tunataka wasomi wenye uwezo mkubwa.
"Hizi siku 16 zitupe fursa katika vyuo vyetu kujadili masula haya, kwa sababu wanafunz afaulu kwa ajili ya kusoma na sio kwa rushwa ya ngono, hata mimi nilipitia huko kwa hiyo ukisema hapana inawezekana sio lazima ukubali," amesema Dkt.Tulia
Pia, Dkt. Tulia amesema jamii iache kuwaona wanawake na watoto wa kike kama viumbe dhaifu hivyo kuwanyanyasa kwa vipigo na kingono, pia amewataka wanaume kuacha kuwapiga wanawake.
"Wanawake waliyoamepewa nafasi kwenye nafasi za maamuzi wameonesha uwezo mkubwa kama ilivyo kwa wanaume hivyo hakuna sababu ya kuwaona ni wadhaifu na kuwapiga,"
Pia, Dkt.Tulia ameitaka jamii kutumia siku hizo 16 kutafakari na kuanzisha mijadala ni kwa namna gani nchi inaweza kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuzungumza na wanafunzi vyuoni na mitaani ili waeleze yanayowakuta.
Aidha, Dkt.Tulia amezindua mfumo wa kutuma taarifa kijinsia (GBV App), ambayo itasaidia watu wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia kutoa taarifa, ambapo ametoa ushauria pia kuwa App hiyo ifike hadi vijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amesema hii ni kampeni ya kitaifa, inaashiria kuwa suala hili la ukatili wa kijinsia lipo duniani kote.
Amesema watu wote wanajukumu la kuhakikisha wanawalea watoto katika mazingira manzuri na pia wanatakiwa kujua kuwa ukatili wa kijinsia ni mbaya ili kupunguza ukatili huo.Dkt. Jingu amesema jibu sahihi la nini kifanyike kukomesha ukatili kwa jamii linatoka kwenye jamii yenyewe, ambapo inaweza kumlinda mwanamke na watoto katika kuhakikisha wanakomesha ukatili huo.
"Tukiwauliza hapa Jeshi la Polisi nini changamoto, watakwambia ipo katika hatua ya kutoa ushahidi mahakamani, wahusika hawaji kwa sababu ya kunlinda mhalifu kwa sababu kosa kama hili la kiukatili ni kosa la kihalifu," amesema Dkt.Jingu
Mkurugenzi wa WiLDAF, Anna Kulaya amesema shirika hilo na wadau wengine wataendelea kutoa wito kwa serikali kuanzisha mchakato wa kutunga sheria kwaajili ya kupambana na ukatili wa kijinsia na mahakama za kifamilia.
Amesema wataendelea kutoa wito wa kuharakisha kupitiwa kwa sheria ya ndoa ya mwaka 1977 ili kuharakishwa usikilizwaji wa mashauri ya ukatili wa majumbani na kuongezewa ulinzi kwa wanawake.
“Ni ombi letu kwa serikali kuu na halmashauri zote kuendelea kutenga fedha za kutosha kwaajili ya utekelezaji wa mpango wa kutokomeza ukatilina tunaishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kusimamia utungwaji wa sera na miongozo thabiti,” alisema
Amesema WiLDAF inatambua juhudi kubwa zilizofanywa na serikali kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na kusaini mikataba ya kimataifa na kikanda inayolinda maslahi na mustakabali wa wanawake.
Kwa upande wa Muwakili wa ubalozi wa Denmark hapa nchini, Metre Spandet na muwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Zlatan Milisic wamesema uko haja ya kutafuta njia mwafaka kwa makundi maalumu ili kuyalinda.
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) akizungumza katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge , Dkt.Tulia Ackson akizundua mfumo wa kutuma taarifa (GBV App) wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF)
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) akizungumza katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia jijini Dar es Salaam.Wageni mbambali wakiwemo Mabalozi hapa nchini na Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Ackson pamoja na Mkurugenzi wa WiLDAF wakifuatilia muendelezo wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia jijini Dar es Salaam.
No comments: